Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili na Mazingira James Lembeli
M WENYEKITI wa Kamati ya Maliasili na Mazingira,
James Lembeli, amesema wanaokamatwa na kuhusishwa na utoroshwaji wa nyara za
serikali nje ya nchi ni vidagaa huku makambare yakiachwa.
Lembeli alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana
na kupongeza juhudi za Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis
Kagasheki, kwa kufanikisha kukamatwa kwa majangili hao.
“Waliokamatwa na wanaoendelea kukamatwa ni vidagaa,
lakini makambare wameachwa, ingawa wanajulikana sasa ni vema wakakamatwa
wahusika wenyewe na sio hao watumwaji,” alisema Lembeli.
Lembeli ambaye pia ni mbunge wa Kahama,
alishauri ni vema operesheni ya Tokomeza Majangiri ikaendelea baada ya
wao kumaliza uchunguzi na kubaini kasoro zilizojitokeza katika operesheni hiyo.
Alisema dunia nzima kwa sasa inapingana na kitendo
cha ujangili na wanaiunga mkono operesheni iliyoanzishwa nchini hivyo ni vema
pia serikali na wadau wengine mbalimbali wakaunga mkono juhudi hizo.
Hivi karibuni shehena yenye urefu wa futi 40
ilinaswa Zanzibar ikiwa na nyara za serikali ambapo hadi sasa watuhumiwa watano
wamekamatwa huku uchunguzi ukiwa unaendelea kubaini wengine.
No comments:
Post a Comment