na
Charles Ndagulla, Moshi-Tanzania daima
WATUHUMIWA
wa ujangili waliokamatwa hivi karibuni katika Operesheni Tokomeza Ujangili
mkoani Kilimanjaro, jana walifikishwa mahakamani mjini hapa akiwamo Mohamed
Hatiki, aliyekutwa na rundo la bunduki na risasi.
Hatiki
anadaiwa kumiliki bunduki sita bila leseni, ambazo ni shotgun namba
TZCAR86629, pistol glock namba RUW605, pistol revolver namba TZCAR 59644,
rifle 375 namba TZCAR93195, rifle 280 namba TZCAR88522 na rifle 22 namba
TZCAR37022.
Hatiki
(26), mkazi wa Kata ya Bondeni, Manispaa ya Moshi na Mohamed Sadiq wa Pasua
walifikishwa juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sophia Massati, huku Sadiq
akizirai akiwa kizimbani baada ya kupata mshituko.
Hatiki,
ambaye ni mshitakiwa wa kwanza anakabiliwa na makosa 15 yanayoangukia chini
ya sheria ya uhifadhi na uhujumu uchumi huku katika shitaka la kwanza
akidaiwa kupatikana na nyara za serikali ambazo ni kwato mbili za kongoni
zenye thamani ya sh milioni 1.04.
Kwa
mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali,
Omari Kibwana, akisaidiana na mwendesha mashitaka kutoka Maliasili, Rusticus
Mahundi, mshitakiwa huyo anadaiwa kupatikana na nyara hizo Oktoba 23, mwaka
huu, alfajiri katika Kata ya Bondeni.
Shitaka
la pili hadi la saba, mshitakiwa anadaiwa kumiliki bunduki sita zilizotajwa
hapo juu bila kuwa na leseni halali.
Shitaka
la nane, Hatiki anadaiwa kupatikana na risasi 23 za bunduki aina ya shotgun
na katika shitaka la tisa anadaiwa kupatikana na risasi saba za bunduki aina
ya pistol glock yenye namba za usajili RUW605 bila leseni.
Katika
shitaka la kumi, Hatiki anadaiwa kupatikana na risasi 56 za bunduki aina ya
pistol revolver bila leseni, wakati shitaka la 11 ni kupatikana na risasi nne
za bunduki aina ya rifle 375 bila leseni.
Mshitakiwa
huyo ambaye yupo nje kwa dhamana, anashitakiwa pia kwa kosa la kukutwa na
maganda ya risasi ya bunduki aina ya rifle 375, risasi 15 za bunduki aina ya
rifle 280, maganda 10 ya bunduki aina ya rifle 280, na risasi 84 za bunduki
aina ya rifle 22.
Naye
mshitakiwa wa pili, Sadiq (67), anakabiliwa na makosa tisa, likiwamo kumiliki
silaha na risasi bila leseni, pamoja na kukutwa na fuvu la nyati na mfupa wa
tembo wenye thamani ya sh milioni 24.1 na tumbili hai mmoja Oktoba 22, mwaka
huu, eneo la Pasua.
Silaha
hizo ni rifle namba TZCAR 82048, rifle MK4, rifle 22, risasi nne za silaha
aina ya shotgun, 12 za bunduki aina ya rifle 303 na 11 za bunduki aina ya
rifle 22.
Hata
hivyo mshitakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na watu
wawili, mmoja aweke dhamana ya fedha taslimu sh milioni 14, hivyo kurejeshwa
rumande hadi Novemba 6, mwaka huu.
|
Friday, November 1, 2013
Abambwa na bunduki sita, shehena ya risasi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment