TEMBO 26 WAHARIBIFU WA MAZAO WALIUAWA SERENGETI.
Serengeti:JUMLA wanyama pori 40 wameuliwa na askari wa idara ya
wanyama pori wilayani Serengeti,kati ya hao 26 ni tembo waharibifu wa mazao na
maisha ya watu kwa kipindi cha toka
mwaka 2006 hadi 2013 .
Kwa mjibu wa taarifa ya
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Goody Pamba kwa wadau wa
uhifadhi waliokutana kujadili athari na mbinu za kukabiliana na tatizo la
uharibifu wa mazao unaofanywa na wanyama waharibifu kwa jamii wanaoishi kando
ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na mapori ya akiba.
Alisema tembo hao wameuliwa
katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo
ambapo kwa mwaka huu tembo 5 wameuawa katika vijiji vya Makundusi na Nyichoka
wakati wa kuwafukuza baada ya kuingia kwenye makazi na mashamba ya wananchi.
Idadi ya Tembo kwenye mabano
walivyouawa,mwaka 2006(2)2008(6)2009(7)2010(6)2011(2)2013(5)mbali na wanyama
hao wapo wengine waliouawa kama kiboko(6)mamba(2)Simba(1) na nyani(5).
Na maeneo ambayo yanavamiwa na
wanyama hao ni Matare,Robanda,Bisarara,Makundusi,Kwitete,Nyichoka,Mbalibali,Manchira,Nyansurura,Nyamakendo,Tamkeri,Nyamburi,Natta,Borenga,Mto
Mara,Park nyigoti,Issenye na Itununu.
Hata hivyo taarifa hiyo ilizua
maswali kutoka kwa wadau mbalimbali kutokana na baadhi ya watumishi wa idara ya
wanyamapori ,kaimu afisa wanyama pori wilaya Cathbert Boma na askari wa idara
hiyo Omar Hussein kukamatwa na kikosi cha operesheni okoa maliasili kwa tuhuma
za ujangili.
Kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi
sasa watu 14 ,ng’ombe 72,mbuzi440,Kondoo 60 wameuliwa,watu 4 wakijeruhiwa
,mashamba 3042 yenye zaidi ya ekari 6,287 yameharibiwa na wanyama hao
hatari,ambao wamepelekea bei ya mahindi kupanda kutoka sh.9,000 hadi sh.14,000
kwa debe la mahindi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment