Kiama
cha majangili chaja
Chanzo
Tanzania Daima.
|
WIZARA
ya Maliasili na Utalii, inakusudia kupeleka sheria mpya bungeni kwa ajili ya
kuwashughulikia majangili na watu wanaojihusisha na uuzaji na usafirishaji wa
meno ya tembo ndani na nje ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
wakati akizungumza kwenye kilele cha Siku ya Utalii Duniani, ambayo kitaifa
ilifanyika kwenye viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza.
Waziri
Nyalandu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele hicho, alisema serikali
imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kudhibiti ujangili na kuongeza kuwa kuna
sheria mpya inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni kwa ajili ya kupata sheria
mpya ya kukabiliana na majangili hao nchini.
Alikiri
kuwapo kwa taarifa za kutajwa baadhi ya vigogo serikalini wanaotuhumiwa
kujihusisha na ujangili wa wanyamapori na uuzaji wa meno ya tembo ndani na
nje ya nchi na kuona yeyote atakayethibitika kujihusisha na ujangili
atachukuliwa hatua za kisheria.
“Sekta
ya utalii nchini ndiyo inayoongoza kuliingizia taifa pato kubwa. Tatizo la
ujangili na uuzaji wa meno ya tembo bado lipo, na wizara imekusudia kupeleka
sheria mpya bungeni ambayo itakuwa kiama cha majangili,” alisema Waziri
Nyalandu.
Aidha,
alisema mbali na sekta ya utalii kuingiza fedha nyingi kwenye pato na uchumi
wa Tanzania, lakini ajira zaidi ya 200 zilizopo nchini zinahusiana na sekta
hiyo, hivyo lazima iwepo sheria kali itakayodhibiti ujambazi wa wanyama.
Katika
hatua nyingine, Nyalandu alikwenda mbali zaidi na kusema kwamba, ana tamani
sana wimbo wa taifa uliopo sasa ubadilishwe na kuwa ule wa ‘Tanzania,
Tanzania, nakupenda kwa moyo wote’, kwani wimbo huo wa ‘Tanzania, Tanzania
nakupenda kwa moyo wote’ unatangaza maajabu ya utalii nchini.
“Wakati
mwingine natamani sana wimbo wa taifa uliopo sasa ubadilishwe na kuwa ule wa
‘Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote.’ Wimbo huu unatangaza maajabu ya
utalii ya hapa kwetu,” alisema.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment