Licha ya Bwawa la Mto Nyange kuwa na vivutio vya asili hakuna mkakati wowote wa kutangaza eneo hilo la utalii na kuiingizia Serikali mapato.
Ni kilometa 123 kutoka Kilwa Masoko yalipo makao
makuu ya Wilaya ya Kilwa. Katika wilaya hiyo kuna Kijiji cha Makangaga
na kuna kivutio kizuri cha utalii kwa mfano viboko wa ajabu ambao
wanatii amri mbalimbali.
Wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 1525
wanaotokana na makabila ya Wamwera, Wangindo, Wamakonde, na Wamachinga
ambao wanalitumia eneo hilo kama kivutio cha utalii ambalo linachangia
pato la wakazi wa eneo hilo mpaka taifa kutokana na watalii wa ndani na
nje.
Viboko wa ajabu
Katika Kijiji cha Makangaga, kilometa tisa kutoka
kijijini hapo, kuna Mto Nyange uliosheheni viboko wa ajabu ambao wana
tabia ya ‘kucheka’ na kutii amri zinazotolewa, hakika ukifika unajua
wamefundishwa, ni fursa nzuri ya utalii kama itatumiwa vyema.
Majira ya usiku viboko hao wanapenda kutembea
kando ya maeneo yao kwa ajili ya kujipatia vyakula na sehemu kubwa
wanakula majani na pia wana tabia za ziada.
Zaidi ya miaka 100 iliyopita mto huo uliotengeneza
bwawa na haukuwa na kiboko hata mmoja, wakazi wa maeneo hayo walitumia
bwawa hilo kwa shughuli za uvuvi na mahitaji ya maji kwa kazi za
kawaida.
Mkazi wa eneo hilo Yahaya Selemani Engema anaeleza
chanzo ni mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Kimombo ambaye alikuwa
mvuvi hodari kwenye bwawa hilo.
Lakini siku moja alipokwenda kuvua hakurejea na historia kuanzia hapo baada ya wananchi kuona kiboko mmoja kwenye bwawa hilo.
“Ndugu zake baada ya kusubiri kwa siku sita
wakiamini atarejea, waliamua kwenda bwawani hapo kwa nia ya kumtafuta,
walimwita kwa kutumia lugha ya kabila la Wamachinga, ajabu baada ya
kutokea Kimombo kama walivyotarajia alitokea kiboko ambaye alicheka kama
ishara ya kuitika, kutokana na hali hiyo ndugu wa familia ya mvuvi huyo
waliamini ndugu yao alizama kwenye bwawa hilo na kubadilika kuwa kiboko
ambao wanatabia ya kucheka,”anasema Omari Yanda mmoja wazee maarufu
kijiini hapo.
Kila mwaka hivi sasa inakadiriwa kuwa wanafikia zaidi ya viboko 300, na kwamba wanatii amri ya ukoo wa Kimombo.
“Familia iliyoshikilia wanyama hao ni ya Kimombo
wanarithishana kwa kuwa kiboko wa kwanza alitoka katika familia hiyo,
wageni wanaofika kuwaona viboko hao huwaita viboko hao kwa kutumia jina
la Kimombo ndipo viboko hao hujitokeza wakicheka,” anasema Yanda.
Miongoni mwa maajabu ya viboko hao ni kuwa wana
uwezo wa kujitokeza pindi wanapohitajika kwa maana wakitakiwa wajitokeze
wadogo wataibuka wadogo na wakitakiwa wajitokeze wazee watajitokeza
wazee wote waliomo bwawani.
Pia tabia nyingine ya ajabu ni kutokuwa waharibifu wa mazao ya wakulima ambayo viboko hao hawafanyi uharibifu wowote wa mazao ya wakulima yanayozunguka katika bwawa hilo.
Pia tabia nyingine ya ajabu ni kutokuwa waharibifu wa mazao ya wakulima ambayo viboko hao hawafanyi uharibifu wowote wa mazao ya wakulima yanayozunguka katika bwawa hilo.
Vilevile hawana madhara kwa binadamu yeyote hata
wakikutana ana kwa ana au wavuvi wanaovua kwenye bwawa hilo hawaguswi au
kuwadhuru. Wavuvi wanaendelea na shughuli za uvuvi bila kujeruhiwa wala
kuuliwa na viboko hao.
Licha ya uwapo wa viboko hao pia eneo hili lina
kivutio kingine kikubwa ambacho ni msitu mnene uliotokana na miti ya
asili na kusababisha eneo hilo kuwa tulivu na mahali pazuri pa
kujipumzisha iwapo patawekewa mazingira rafiki hii inatokana na
kutokatwa miti.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Makangaga, Muhidini
Mkungula alisema eneo hilo lipo kwenye usimamizi wa kijiji na uongozi wa
kijiji umeweka mkakati wa kuulinda msitu huo na kuwachukulia hatua kali
wale wanafanya uaharibifu wa kukata miti.
“Tunashukuru wananchi wetu wanatoa ushirikiano katika utunzaji wa msitu huu”anasema Mkungula.
Tambiko la jadi
Wenyeji wa vijiji hivyo kwa imani ya viboko hao
wanalitumia eneo la bwawa la Mto Nyange kwa shughuli za jadi na kila
mwaka huenda siku maalumu na wenyeji hao wanapika pombe za kiasili na
kucheza ngoma za kiasili, kunywa pombe hiyo na kufanya tambiko kubwa kwa
lengo la kuomba mizimu.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Makangaga Said Ali
Kilete anasema licha ya tambiko hilo la kila mwaka pia wananchi wa
maeneo yanayozunguka eneo hilo wanatumia eneo hilo kwa maombi maalumu
akitolea mfano iwapo kunajitokeza tatizo la ukame wananchi wanaomba mvua
kwa kutumia eneo hilo.
Serikali inasemaje?
Licha ya eneo hili kuwa na vivutio bado Serikali
haina mkakati wowote wa kulifanya kuwa ni moja ya maeneo yatakayochangia
pato la taifa au kuwa eneo la kitalii.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdalah Ulega anaeleza
kwamba licha ya kupata taarifa ya eneo hilo, wilaya haina mkakati wowote
wa kuendeleza na kulitangaza na kuwa sehemu maalumu ya utalii.
Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii nchini, Godfrey
Tengeneza anaeleza kwamba Bodi ya utalii inatambua eneo hilo na maeneo
mengine wilayani Kilwa yenye vivutio ambavyo ni vya kitalii na kwamba
hivi sasa bodi hiyo imeanza kuvitangaza vyanzo hivyo.
Anasema wameanza kutangaza vyanzo hivyo lakini hivi sasa eneo hawajaweka mkakati wote wa kutangaza viboko wa ajabu.
Anasema wameanza kutangaza vyanzo hivyo lakini hivi sasa eneo hawajaweka mkakati wote wa kutangaza viboko wa ajabu.
“Kilwa ina vivutio vingi ambavyo vinatosha kuwa
vya kitalii na hivi sasa bodi inaanza kuviwekea mikakati ili vivutir
watalii,”anasema Tengeneza.
No comments:
Post a Comment