Thursday, June 27, 2013

Kukosa ushirikiano chanzo cha utalii kusuasua























Nchi nyingi zinazoendelea duniani, zimetengeneza sera kuboresha sekta ya utalii kama njia ya
kukabiliana na umaskini.Wataalamu wanasema sera peke yake haiwezi kuboresha sekta ya utalii
nchini na kutokana na hali hiyo Serikali inatakiwa kuchukua hatua kadhaa, kuondoa vikwazo
vilivyopo katika sekta hiyo kama inataka kuvutia utalii na kuwa namba moja Afrika Mashariki
na Bara Afrika.Moja ya viwakwazo ni sekta hiyo kushindwa kushirikiana na wadau wengine
wa utalii.Ushirikiano ni muhimu
Miongoni mwa mambo ambayo yametajwa na wataalamu hao kusaidia kuimarisha sekta ya utalii ni
ushirikiano kati ya wadau wa utalii na Serikali.Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda, Biashara
na Kilimo, Tawi la Arusha , Adolf Olomi anaamini kwamba kwa kushirikiana, itapatikana suluhu za
changamoto zinazokwamisha sekta hiyo.Ushirikiano huo pia utasaidia kuwapo kwa mikutano yenye
 ushawishi kwa Serikali na kuharakisha mchakato wa kuoanisha sheria kwenye itifaki inayoanzisha
Soko la Pamoja la Afrika Mashariki (ACCMP).

Utafiti kuhusu utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja nchini Tanzania kwenye sekta ya utalii,
wataalamu walishauri wadau katika sekta ya utalii kujenga hoja na kuambatanisha na ushahidi kabla ya
 kukutana na mamlaka za Serikali ili kupatiwa msaada badala ya kubaki kunung’unika tu.
“Kutegemeana na suala lililopo, Myororo wa Thamani wa Wadau wa Utalii Tanzania (TVC) na wengine
 wanaofanya shughuli za utalii watafaidika na kushawishi wabunge kuishawishi Serikali kufanya mabadiliko
yaliyopendekezwa kwa lengo la kuboresha sekta ya utalii,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Tanzania inatakiwa kutengeneza muktadha wa utalii ambao utakuwa ndiyo
 dira ya miundombinu inayotakiwa kufanikisha sekta ya utalii.
Hali ya sasa si nzuri hasa ukizingatia taarifa ya mwaka 2011 kuhusu utalii duniani na Tanzania imekuwa ni
nchi ya 127 kati ya nchi 139 ambazo zina mazingira bora ya utalii ingawa ina vivutio vingi na bora zaidi
duniani.“Ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma utasaidia ushawishi kwa Serikali kuona umuhimu wa
kuboresha miundombinu ya sekta ya utalii.

 “Chama cha biashara ya utalii, kikishirikiana na wadau wengine kama TCCIA na Shirikisho la Wenye
Viwanda (CTI), ni lazima kuishirikisha TPSF kupitia BEST-AC kuangalia namna ya kupunguza changamoto
za uwekezaji sekta ya utalii,” inasema ripoti ya World Economic Forum ya mwaka 2011.
TVC kupitia nafasi zao ni vyema wakawa na uhusiano wa karibu na BEST – AC, taasisi ya Serikali Ofisi
ya Waziri Mkuu yenye lengo la kufanikisha mazingira bora ya kufanyia biashara kwa masilahi ya wajasiriamali,
 Serikali na walaji.
Uhusiano huo utasaidia kuishawishi Serikali kutekeleza mapendekezo ambayo yameshauriwa katika baadhi ya
 tafiti mbalimbali zenye lengo la kuboresha sekta ya utalii.“Pia wadau wa utalii wanaweza kuchambua mawazo
 ya nchi za Afrika Mashariki kuhusu namna ya kushawishi Serikali kujikita zaidi kutatua changamoto
zinazokabili sekta hiyo,” inasema ripoti hiyo.Mbali na hayo umefika wakati TVC kuoanishwa na taarifa ya
CIBER ya Desemba 2010 ili kuwa na mfumo wa kudumu wa ushirikiano.
CTI, Tawi la Arusha miaka ya hivi karibuni ilifanya utafiti kuhusiana na TVC na kutoa ripoti ambayo
 iliyobatizwa CIBER na mapendekezo kadhaa.“Kwa utekelezaji wa pamoja, kutafanya sekta ya utalii
kupanda na kuwa namba mbili kwa vivutio duniani, kushawishi watalii wengi na kupata mapato zaidi,”
 inaeleza ripoti hiyo.Pamoja na kwamba sekta ya utalii ni ya pili kwa kuingiza fedha za kigeni, sekta hiyo
 ina tatizo katika uwekezaji na uanzishaji wa shughuli za utalii.
Kwa kuwa huenda itachukua muda mrefu itifaki ya soko la pamoja la Afrika Mashariki kutekelezwa, ni
vyema serikali ikafanya mabadiliko yanayotakiwa kwenye sekta ya utalii.
Olomi anasema:”Baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanywa, hayana gharama kwa serikali au kupoteza
kipato chake, mambo hayo yanarekebisha mwenendo wa sekta ya utalii na kuiweka mahali inapostahili.”
Mathalan nchini Kenya Mathalan nchini Kenya mtu anayetaka kuanzisha biashara ya kusafirisha watalii hahitaji
 kumiliki gari kupewa leseni, lakini Tanzania ni lazima.

« Previous Page 1 | 2 | 3
 Kwa kuwa na utaratibu kama huo hautainyima Serikali mapato kwani mahitaji ya magari yapo na si lazima
anayesafirisha watalii kuwa na kampuni bali anaweza kukodisha na kufanya biashara hiyo vizuri.
Tujadiliane kupitia Ujumbe mfupi SMS kwa 15774 ukianza na neno BIZ na kufuatia ujumbe wako.
Ujumbe wako mfupi ni Bure, hautozwi

No comments:

Post a Comment