Thursday, June 27, 2013

Kukosa ushirikiano chanzo cha utalii kusuasua























Nchi nyingi zinazoendelea duniani, zimetengeneza sera kuboresha sekta ya utalii kama njia ya
kukabiliana na umaskini.Wataalamu wanasema sera peke yake haiwezi kuboresha sekta ya utalii
nchini na kutokana na hali hiyo Serikali inatakiwa kuchukua hatua kadhaa, kuondoa vikwazo
vilivyopo katika sekta hiyo kama inataka kuvutia utalii na kuwa namba moja Afrika Mashariki
na Bara Afrika.Moja ya viwakwazo ni sekta hiyo kushindwa kushirikiana na wadau wengine
wa utalii.Ushirikiano ni muhimu
Miongoni mwa mambo ambayo yametajwa na wataalamu hao kusaidia kuimarisha sekta ya utalii ni
ushirikiano kati ya wadau wa utalii na Serikali.Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda, Biashara
na Kilimo, Tawi la Arusha , Adolf Olomi anaamini kwamba kwa kushirikiana, itapatikana suluhu za
changamoto zinazokwamisha sekta hiyo.Ushirikiano huo pia utasaidia kuwapo kwa mikutano yenye
 ushawishi kwa Serikali na kuharakisha mchakato wa kuoanisha sheria kwenye itifaki inayoanzisha
Soko la Pamoja la Afrika Mashariki (ACCMP).

Utafiti kuhusu utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja nchini Tanzania kwenye sekta ya utalii,
wataalamu walishauri wadau katika sekta ya utalii kujenga hoja na kuambatanisha na ushahidi kabla ya
 kukutana na mamlaka za Serikali ili kupatiwa msaada badala ya kubaki kunung’unika tu.
“Kutegemeana na suala lililopo, Myororo wa Thamani wa Wadau wa Utalii Tanzania (TVC) na wengine
 wanaofanya shughuli za utalii watafaidika na kushawishi wabunge kuishawishi Serikali kufanya mabadiliko
yaliyopendekezwa kwa lengo la kuboresha sekta ya utalii,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Tanzania inatakiwa kutengeneza muktadha wa utalii ambao utakuwa ndiyo
 dira ya miundombinu inayotakiwa kufanikisha sekta ya utalii.
Hali ya sasa si nzuri hasa ukizingatia taarifa ya mwaka 2011 kuhusu utalii duniani na Tanzania imekuwa ni
nchi ya 127 kati ya nchi 139 ambazo zina mazingira bora ya utalii ingawa ina vivutio vingi na bora zaidi
duniani.“Ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma utasaidia ushawishi kwa Serikali kuona umuhimu wa
kuboresha miundombinu ya sekta ya utalii.

 “Chama cha biashara ya utalii, kikishirikiana na wadau wengine kama TCCIA na Shirikisho la Wenye
Viwanda (CTI), ni lazima kuishirikisha TPSF kupitia BEST-AC kuangalia namna ya kupunguza changamoto
za uwekezaji sekta ya utalii,” inasema ripoti ya World Economic Forum ya mwaka 2011.
TVC kupitia nafasi zao ni vyema wakawa na uhusiano wa karibu na BEST – AC, taasisi ya Serikali Ofisi
ya Waziri Mkuu yenye lengo la kufanikisha mazingira bora ya kufanyia biashara kwa masilahi ya wajasiriamali,
 Serikali na walaji.
Uhusiano huo utasaidia kuishawishi Serikali kutekeleza mapendekezo ambayo yameshauriwa katika baadhi ya
 tafiti mbalimbali zenye lengo la kuboresha sekta ya utalii.“Pia wadau wa utalii wanaweza kuchambua mawazo
 ya nchi za Afrika Mashariki kuhusu namna ya kushawishi Serikali kujikita zaidi kutatua changamoto
zinazokabili sekta hiyo,” inasema ripoti hiyo.Mbali na hayo umefika wakati TVC kuoanishwa na taarifa ya
CIBER ya Desemba 2010 ili kuwa na mfumo wa kudumu wa ushirikiano.
CTI, Tawi la Arusha miaka ya hivi karibuni ilifanya utafiti kuhusiana na TVC na kutoa ripoti ambayo
 iliyobatizwa CIBER na mapendekezo kadhaa.“Kwa utekelezaji wa pamoja, kutafanya sekta ya utalii
kupanda na kuwa namba mbili kwa vivutio duniani, kushawishi watalii wengi na kupata mapato zaidi,”
 inaeleza ripoti hiyo.Pamoja na kwamba sekta ya utalii ni ya pili kwa kuingiza fedha za kigeni, sekta hiyo
 ina tatizo katika uwekezaji na uanzishaji wa shughuli za utalii.
Kwa kuwa huenda itachukua muda mrefu itifaki ya soko la pamoja la Afrika Mashariki kutekelezwa, ni
vyema serikali ikafanya mabadiliko yanayotakiwa kwenye sekta ya utalii.
Olomi anasema:”Baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanywa, hayana gharama kwa serikali au kupoteza
kipato chake, mambo hayo yanarekebisha mwenendo wa sekta ya utalii na kuiweka mahali inapostahili.”
Mathalan nchini Kenya Mathalan nchini Kenya mtu anayetaka kuanzisha biashara ya kusafirisha watalii hahitaji
 kumiliki gari kupewa leseni, lakini Tanzania ni lazima.

« Previous Page 1 | 2 | 3
 Kwa kuwa na utaratibu kama huo hautainyima Serikali mapato kwani mahitaji ya magari yapo na si lazima
anayesafirisha watalii kuwa na kampuni bali anaweza kukodisha na kufanya biashara hiyo vizuri.
Tujadiliane kupitia Ujumbe mfupi SMS kwa 15774 ukianza na neno BIZ na kufuatia ujumbe wako.
Ujumbe wako mfupi ni Bure, hautozwi

TANZANIA: Viboko wa ajabu wasiojulikana kwa watalii



Viboko wakijidai majini 

Licha ya Bwawa la Mto Nyange kuwa na vivutio vya asili hakuna mkakati wowote wa kutangaza eneo hilo la utalii na kuiingizia Serikali mapato.
Ni kilometa 123 kutoka Kilwa Masoko yalipo makao makuu ya Wilaya ya Kilwa. Katika wilaya hiyo kuna Kijiji cha Makangaga na kuna kivutio kizuri cha utalii kwa mfano viboko wa ajabu ambao wanatii amri mbalimbali.
Wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 1525 wanaotokana na makabila ya Wamwera, Wangindo, Wamakonde, na Wamachinga ambao wanalitumia eneo hilo kama kivutio cha utalii ambalo linachangia pato la wakazi wa eneo hilo mpaka taifa kutokana na watalii wa ndani na nje.
Viboko wa ajabu
Katika Kijiji cha Makangaga, kilometa tisa kutoka kijijini hapo, kuna Mto Nyange uliosheheni viboko wa ajabu ambao wana tabia ya ‘kucheka’ na kutii amri zinazotolewa, hakika ukifika unajua wamefundishwa, ni fursa nzuri ya utalii kama itatumiwa vyema.
Majira ya usiku viboko hao wanapenda kutembea kando ya maeneo yao kwa ajili ya kujipatia vyakula na sehemu kubwa wanakula majani na pia wana tabia za ziada.
Zaidi ya miaka 100 iliyopita mto huo uliotengeneza bwawa na haukuwa na kiboko hata mmoja, wakazi wa maeneo hayo walitumia bwawa hilo kwa shughuli za uvuvi na mahitaji ya maji kwa kazi za kawaida.
Mkazi wa eneo hilo Yahaya Selemani Engema anaeleza chanzo ni mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Kimombo ambaye alikuwa mvuvi hodari kwenye bwawa hilo.
Lakini siku moja alipokwenda kuvua hakurejea na historia kuanzia hapo baada ya wananchi kuona kiboko mmoja kwenye bwawa hilo.
“Ndugu zake baada ya kusubiri kwa siku sita wakiamini atarejea, waliamua kwenda bwawani hapo kwa nia ya kumtafuta, walimwita kwa kutumia lugha ya kabila la Wamachinga, ajabu baada ya kutokea Kimombo kama walivyotarajia alitokea kiboko ambaye alicheka kama ishara ya kuitika, kutokana na hali hiyo ndugu wa familia ya mvuvi huyo waliamini ndugu yao alizama kwenye bwawa hilo na kubadilika kuwa kiboko ambao wanatabia ya kucheka,”anasema Omari Yanda mmoja wazee maarufu kijiini hapo.
Kila mwaka hivi sasa inakadiriwa kuwa wanafikia zaidi ya viboko 300, na kwamba wanatii amri ya ukoo wa Kimombo.
“Familia iliyoshikilia wanyama hao ni ya Kimombo wanarithishana kwa kuwa kiboko wa kwanza alitoka katika familia hiyo, wageni wanaofika kuwaona viboko hao huwaita viboko hao kwa kutumia jina la Kimombo ndipo viboko hao hujitokeza wakicheka,” anasema Yanda.
Miongoni mwa maajabu ya viboko hao ni kuwa wana uwezo wa kujitokeza pindi wanapohitajika kwa maana wakitakiwa wajitokeze wadogo wataibuka wadogo na wakitakiwa wajitokeze wazee watajitokeza wazee wote waliomo bwawani.

 Pia tabia nyingine ya ajabu ni kutokuwa waharibifu wa mazao ya wakulima ambayo viboko hao hawafanyi uharibifu wowote wa mazao ya wakulima yanayozunguka katika bwawa hilo.

Vilevile hawana madhara kwa binadamu yeyote hata wakikutana ana kwa ana au wavuvi wanaovua kwenye bwawa hilo hawaguswi au kuwadhuru. Wavuvi wanaendelea na shughuli za uvuvi bila kujeruhiwa wala kuuliwa na viboko hao.
Licha ya uwapo wa viboko hao pia eneo hili lina kivutio kingine kikubwa ambacho ni msitu mnene uliotokana na miti ya asili na kusababisha eneo hilo kuwa tulivu na mahali pazuri pa kujipumzisha iwapo patawekewa mazingira rafiki hii inatokana na kutokatwa miti.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Makangaga, Muhidini Mkungula alisema eneo hilo lipo kwenye usimamizi wa kijiji na uongozi wa kijiji umeweka mkakati wa kuulinda msitu huo na kuwachukulia hatua kali wale wanafanya uaharibifu wa kukata miti.
“Tunashukuru wananchi wetu wanatoa ushirikiano katika utunzaji wa msitu huu”anasema Mkungula.
Tambiko la jadi
Wenyeji wa vijiji hivyo kwa imani ya viboko hao wanalitumia eneo la bwawa la Mto Nyange kwa shughuli za jadi na kila mwaka huenda siku maalumu na wenyeji hao wanapika pombe za kiasili na kucheza ngoma za kiasili, kunywa pombe hiyo na kufanya tambiko kubwa kwa lengo la kuomba mizimu.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Makangaga Said Ali Kilete anasema licha ya tambiko hilo la kila mwaka pia wananchi wa maeneo yanayozunguka eneo hilo wanatumia eneo hilo kwa maombi maalumu akitolea mfano iwapo kunajitokeza tatizo la ukame wananchi wanaomba mvua kwa kutumia eneo hilo.
Serikali inasemaje?
Licha ya eneo hili kuwa na vivutio bado Serikali haina mkakati wowote wa kulifanya kuwa ni moja ya maeneo yatakayochangia pato la taifa au kuwa eneo la kitalii.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdalah Ulega anaeleza kwamba licha ya kupata taarifa ya eneo hilo, wilaya haina mkakati wowote wa kuendeleza na kulitangaza na kuwa sehemu maalumu ya utalii.
Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii nchini, Godfrey Tengeneza anaeleza kwamba Bodi ya utalii inatambua eneo hilo na maeneo mengine wilayani Kilwa yenye vivutio ambavyo ni vya kitalii na kwamba hivi sasa bodi hiyo imeanza kuvitangaza vyanzo hivyo.

  Anasema wameanza kutangaza vyanzo hivyo lakini hivi sasa eneo hawajaweka mkakati wote wa kutangaza viboko wa ajabu.

“Kilwa ina vivutio vingi ambavyo vinatosha kuwa vya kitalii na hivi sasa bodi inaanza kuviwekea mikakati ili vivutir watalii,”anasema Tengeneza.

Wednesday, June 26, 2013

TUZO ZA WAANDISHI MAHIRI WA HABARI ZA UTALII NA MALIASILI ZILIZOANDALIWA NA TANAPA

 WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KHAMISI KAGASHEKI AKIMKABIDHI MWANDISHI WA MAGAZETI YA KAMPUNI YA MWANANCHI MUSSA JUMA AMBAYE PIA NI NAIBU KATIBU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MALIASILI NA UTALII,HUNDI YA SH,MIL.1 BAADA YA KUIBUKA MSHINDI WA PILI WA UANDISHI WA HABARI ZA UHIFADHI ,SHINDANO LILILOANDALIWA NA TANAPA,HAFLA HIYO IMEFANYIKA UKUMBI WA HILL TOP MJINI IRINGA.
 ZAWADI HIZO ZILITOLEWA KWA WAANDISHI MBALIMBALI ,ZAWADI YA KWANZA IKIWA NI SH.MIL.1.5 NA SAFARI YA KUJIFUNZA MAMBO YA UTALII KATIKA NCHI ZA SADC
 MCHAKATO HUO ULISHIRIKISHA VIONGOZI WAANDAMIZI WA TANAPA ,NA WABUNGE
 MWANDISHI WA NIPASHE AMEIBUKA MSHINDI WA KWANZA NA KUJIZOLEA KITITA CHA SH,MIL.1.5 NA SAFARI KTK NCHI ZA SADC.
HAPO MSHINDI ANATAKIWA KUTANGAZWA.

Tuesday, June 25, 2013

WAHARIRI/WAANDISHI WAANDAMIZI WAWEKA MAAZIMIO YA KUPAMBANA NA UJANGILI WA TEMBO MJINI IRINGA

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na maofisa Wanyamapori katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma limekamata meno ya tembo 18 yenye thamani ya sh milioni 216.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, alisema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Nsimeki alisema kuwa tukio hilo limetokea Juni 20, mwaka huu majira ya saa tisa usiku nje kidogo ya Kijiji cha Majala, Kata ya Nandepo, katika Wilaya ya Tunduru, ambapo askari polisi wakiwa doria waliwaona watu wanne wakisukuma baiskeli zao kuelekea katika kijiji hicho.
Kamanda Nsimeki alisema watu hao walipoona mwanga wa taa za gari la polisi walishtuka na kuzitupa baiskeli zao nne zilizokuwa zimebeba vifurushi na kukimbia.
Alisema askari walipofika eneo zilipotupwa baiskeli hizo na mizigo yake waligundua kuwa ni meno ya tembo 18 yenye uzito wa kilo 84, ambazo zinakadiriwa kuwa na thamani ya sh milioni 216.
Kamanda Nsimeki alisema jeshi hilo mpaka sasa halimshikilii mtu yeyote kuhusu sakata hilo lakini linaendelea na jitihada za kuwatafuta waliozitelekeza baiskeli hizo.
Alisema katika kipindi hiki kifupi polisi wamekamata meno ya tembo kwa wingi na tukio hili ni la tano na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa taarifa za siri kwa jeshi hilo.
Aliongeza kusema kuwa mafanikio hayo ya kuwakamata waalifu pamoja na majangili mkoani humo kunatokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na watendaji wa jeshi hilo.
Kamanda Nsimeki alisema vita ya kupambana na wawindaji na wafanyabiashara ya meno ya tembo au rasilimali nyingine za taifa zinahitaji ushirikiano wa kila mwananchi.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Songea wameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa zawadi kwa wasamaria wema wanaotoa taarifa sahihi za kuwafichua watu wanaojihusisha na biashara ya meno ya tembo.


 MENEJA UHUSIANO WA TANAPA PASCHAEL SHELUTETE AKITOA UFAFANUZI JUU YA SEMINA YA WAHARIRI WA HABARI/WAANDISHI WAANDAMIZI DHIMA IKIWA NI UMUHIMU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUPAMBANA NA UJANGILI WA TEMBO,UKUMBI WA SIASA NI KILIMO MJINI IRINGA







BAADHI WA WASHIRIKI WAKIFUATILIA MAELEZO YA UTANGULIZI
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMISI KAGASHEKI KATIKATI,KUSHOTO KWAKE NI JAMES LEMBELI MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI MALIASILI NA MAZINGIRA,MCHUNGAJI PETER MSIGWA WAZIRI KIVULI NA KULIA KWAKE NI RC IRINGA DK CHRISTINE ISHENGOMA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO