Na Waandishi wetu
19th August 2015
Mwaka jana utafiti ulionyesha kuwa Tanzania
imepoteza zaidi ya nusu ya tembo wake.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dk. Adelhelm Meru.
Ujangili uliokithiri nchini Tanzania,
unatishia kudhoofisha uchumi wa nchi ambao unazidi kukua.
Sekta ya utalii ina mchango mkubwa
kwenye pato la taifa na katika kuongeza ajira.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dk. Adelhelm Meru, ameonya kwamba kuna uwezekano ujangili ukaathiri
ajira takriban milioni 3.8 kwenye sekta ya utalii katika ukanda wa Afrika
Mashariki wakiwamo waongoza watalii, madereva, na hoteli na wahudumu wa
migahawa. Kwa mujibu wa shirika la All Africa Tanzania pamoja na nchi nyingine
barani Afrika zimeathirika mno kutokana na ujangili katika miaka 10
iliyopita.
Mwaka jana, utafiti ulionyesha kuwa
Tanzania imepoteza zaidi ya nusu ya tembo wake ambapo idadi imepungua kutoka
tembo 110,000 mwaka 2009 kufikia chini ya tembo 44,000.
Alisema Tanzania ina ajira 700,000
kutokana na idadi hiyo inaweza kuongezeka mara mbili endapo ujangili
uliokithiri kwa wanyamapori utaisha.
Katika kuisaidia Serikali ya
Tanzania, hivi karibuni mashirika ya Wildaid na African Wildlife Foundation,
yalizindua kampeni mpya ijulikanayo kama `Ujangili Unatuumiza Sote’ kwa
kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Utafiti uliofanywa na WildAid kwa
kushirikiana na African Wildlife Foundation kwa kuwahoji Watanzania zaidi ya
2,000 waishio mijini na vijijini, uligundua kwamba asilimia 80 kati yao
wanaelewa madhara yanayoweza kuikumba Tanzania endapo tembo watatoweka.
Kati ya walihojiwa katika utafiti
huo, asilimia 73 walisema wanyama pori ni mojawapo ya alama za taifa na urithi
wa taifa.
Kwa
upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wildaid, Peter Knights, alisema: “Ujangili
kwa tembo ni wizi unaowaumiza Watanzania wa sasa na wa vizazi vijavyo.”
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment