Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu
Na Goodluck Eliona
Posted Jumatano,Mei6 2015 saa 10:40 AM
Posted Jumatano,Mei6 2015 saa 10:40 AM
Kwa ufupi
Juzi, Waziri Nyalandu na watendaji
wake waliwasilisha bajeti ya wizara kwa kamati hiyo, lakini baada ya wajumbe
kuipitia walibaini kuwa haikufanyiwa marekebisho kadhaa, yakiwamo mabadiliko ya
tozo za ada ya kuingia kwenye hifadhi za Taifa kama walivyokuwa wamependekeza
awali.
Dar es Salaam. Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Maliasili na Mazingira imemwongezea muda Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu kuifanyia marekebisho bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka
2015/2016 iliyokataliwa baada ya kubainika kuwa na kasoro kadhaa.
Juzi, Waziri Nyalandu na watendaji
wake waliwasilisha bajeti ya wizara kwa kamati hiyo, lakini baada ya wajumbe
kuipitia walibaini kuwa haikufanyiwa marekebisho kadhaa, yakiwamo mabadiliko ya
tozo za ada ya kuingia kwenye hifadhi za Taifa kama walivyokuwa wamependekeza
awali.
Waziri Nyalandu alipewa siku moja
kufanya marekebisho na kisha kuiwasilisha upya bajeti hiyo jana. Hata hivyo,
akizungumza mbele ya kamati jana, Nyalandu alisema muda aliokuwa amepewa
haukutosha ndipo Lembeli alipoongeza muda hadi Mei 14 mwaka huu.
“Tunawapa muda hadi Mei 14, Kamati
itakutana na nyinyi kule Dodoma mje mkiwa mmefanya marekebisho,” alisema Lembeli.
Lembeli alisema kamati yake
haitapitisha bajeti hiyo hadi itakapojiridhisha kuwa mapendekezo yote
yaliyotolewa yamefanyiwa kazi. Alitaja mapendekezo hayo kuwa ni pamoja na
Nyalandu kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya Arusha iliyotaka kuanza mara moja kwa
utekelezwaji wa tozo mpya za kuingia kwenye hifadhi za Taifa.
Pia, Lembeli alisema waziri huyo
alishauriwa asibadilishe mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan kutokana na
mgogoro uliokuwapo, badala yake alikata kipande cha ardhi na kukigawa kwa
mwekezaji kinyume cha sheria.
Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa
Kahama, aliongeza kuwa Nyalandu amebadilisha tozo za ada kwa watalii wanaoingia
kwenye hifadhi na kuwaruhusu wanaotoka nje ya hifadhi kurejea bila kulipa ada
upya. Katika maagizo ya awali, mtalii anayetoka ndani ya hifadhi alitakiwa
kulipa ada kila anapoingia tena.
Kwa mujibu wa kamati hiyo, ada
nyingine zilizofutwa ni zilizokuwa zinatozwa katika kambi za wageni na
wafanyakazi. Alipoulizwa kuhusu ada hizo, Nyalandu alisema angepandisha ada
hizo Julai mwaka huu, jambo ambalo lilipingwa na wajumbe wa kamati.
Hata hivyo, Lembeli alisema kuwa
viwango hivyo vilitakiwa kupandishwa tangu Aprili Mosi mwaka huu na kwamba
tangu wakati huo Waziri Nyalandu ameiingizia Serikali hasara ya Sh15 bilioni
No comments:
Post a Comment