Tuesday, January 6, 2015

WALAANI MAUAJI YA SIMBA.



Na Mwandishi wetu
Januari  5,2014.


 Baadhi ya mizoga ya Simba waliouawa katika enep la hifadhi ya jamii ya Ikona Wma kwa kitu kinachodaiwa sumu,jumla ya simba 6 waliuawa.picha na Journo.
 
Arusha,Chama cha Waandishi wa habari za Maliasili na utalii Tanzania
Tourism&Natural Resources Journalist Centre(TJT) na chama cha marafiki
wa wanyama wakubwa(The Friends of Big Five), wamelaani kitendo cha
kuuawa simba sita  katika kijiji cha Olasiti jirani na hifadhi ya
Taifa ya Tarangire na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.

Tukio hilo ni la pili  kubwa kutokea ambapo oktoba 30,2014 simba sita
waliuawa kwa kitu kinachodaiwa kuwa sumu katika eneo la hifadhi ya
Jamii ya Ikona Wma wilayani Serengeti ,baada ya kudaiwa kuua ng’ombe
wa mfugaji mmoja.

Mkurugenzi wa habari wa TJT, Anthony Mayunga alisema jana kuwa,
matukio ya  kuuawa Simba sita  kinaonesha ni jinsi gani watu ambao
wanaishi jirani na maeneo ya hifadhi wasivyothamini wanyamapori hasa
Simba.

Mayunga alisema, ili kuonesha kuna umuhimu wa kulindwa na kuhifadhiwa
wanyama hao, serikali inapaswa kufanya uchunguzi na kuwabaini wahusikana kuwachukulia hatua.

"matukio ya kuuawa Simba nje ya hifadhi za Taifa  yamekuwa yakitokea
mara kwa mara hivyo…Simba sita waliuawa Serengeti na Tarangire
sita,lakini mauaji ya wanyama hao ambao wanazidi kupungua yanaongezeka,ili kulinda wanyama hao  umefika wakati matukio haya

yakakomeshwa"alisema.

Naye Mwenyekiti wa Friends of Big Five, Shermark Ngahemera  alisema
umefika wakati, wananchi wanaoishi jirani na hifadhi kupewa elimu ya
kutosha juu ya kulindwa wanyama ambao wapo hatarini kutoweka.
Ngahemera alisema, katika hifadhi nyingi sasa kuna upungufu mkubwa wa
Simba na maeneo mengine wanyama hao  wamekwisha hivyo ni muhimu sanawadau kushirikiana kubainisha faida za ulinzi na wanyamapori.

"ni muhimu tafiti na uchunguzi ufanywe katika maeneo haya ni kubanisha
chanzo cha migogoro na hatua stahiki kumalizwa ili kuendelea
kuhifadhiwa wanyamapori hapa nchini"alisema.

Alisema wanyama wakubwa kama Simba, Tembo, Faru, Nyati na Chui maisha yao yapo  hatarini kutokana na kuuawa na majangili na  wananchi kwa manufaa yao hivyo ni muhimu wakalindwa kwa gharama zote.


Simba ni miongoni mwa wanyama ambao, wamekuwa wakiliingizia taifa
fedha nyingi za kigeni, kutokana  na kuwa moja ya vivutio vikubwa vya
watalii wanaotembelea hifadhi za Taifa,mapori ya akiba na hifadhi za
Jamii(Wma)
mwisho.

No comments:

Post a Comment