Monday, May 5, 2014

Majangili wazidi kuteketeza tembo Tarangire




Na Keku Lazaro, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Mei5  2014  saa 11:17 AM
Kwa ufupi
Imeelezwa kuwa hiyo inaonyesha kwamba hali ya ujangili katika hifadhi mbalimbali nchini inaendelea na kusababisha kupotea kwa wanyama hao.
Manyara. Tembo wanane katika Hifadhi ya Tarangire mkoani hapa wameuawa katika kipindi cha Novemba 2013 hadi sasa huku meno 17 ya tembo yakikamatwa katika operesheni inayoendelea kufanywa na askari wa hifadhi hiyo.
Imeelezwa kuwa hiyo inaonyesha kwamba hali ya ujangili katika hifadhi mbalimbali nchini inaendelea na kusababisha kupotea kwa wanyama hao.
Mhifadhi mkuu wa Tarangire, Stefano Qolli aliwaambia waandishi wa habari kuwa ujangili bado haujakoma.
Qolli alisema kuuawa kwa tembo hao kunatokana na watu wanaodhaniwa kuwa ni majangili kutoka katika vijiji vya jirani kuwawekea mitego mbalimbali tembo hao ikiwamo maboga yenye sumu na hali hiyo imesababisha kupungua kwa idadi ya wanyama hao Tarangire.
Alitaja mbinu nyingine iliyoua tembo hao wanane kuwa ni ile ya kuwatega kwa kamba.
Mbali na hayo alisema jumla ya meno 17 ya tembo yalikamatwa.
yalitokea katika vijiji vinne ambavyo ni Kiteto,Kibao cha Manyara Ranch, Marangw, pamoja na Kondoa.
“Kupatikana kwa meno haya ya tembo kunatokana na taarifa tulizopata kutoka kwa raia wema pamoja na askari wa kikosi dhidi ya ujangili, lakini pia bado tunaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika wanafikishwa katika vyombo vya dola,” alisema mhifadhi huyo.
Kutokana na mauji hayo ya tembo pamoja na meno yake jumla ya majangili 25 walikamatwa kwa kipindi cha November 2013 hadi sasa na tayari hatua za kisheria zimeshachukuliwa ikiwamo kufikishwa mahakamani ingawaje kesi zao bado zinaendelea.

Friday, May 2, 2014

Nyalandu amtimua Mkurugenzi Wanyamapori Kamati ya Bunge



Lazaro Nyalandu 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Mei2  2014  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Nyalandu alikiri kumzuia Songorwa kujitambulisha: “Kwanza sikujua kama angekuwapo katika kikao kile, maana suala lake bado hatujalizungumza ofisini.
Dar es Salaam. Hatua ya kurejeshwa kazini Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa baada ya kutimuliwa kazi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu imeibua mapya baada ya mkurugenzi huyo kutimuliwa katika Kamati ya Bunge jana.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira walikubaliana na pendekezo la Nyalandu kutaka Profesa Songorwa asijitambulishe katika kikao cha kamati hiyo kwa kuwa hakuwa anatambulika.
Sakata hilo lilitokea wakati kigogo huyo na watendaji wengine walipokuwa wakijitambulisha kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati hiyo kilichokuwa kikijadili Bajeti ya Serikali mwaka 2014/15.
Februari mwaka huu, Profesa Songorwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Jafari Kidegesho walisimamishwa kazi na Nyalandu akisema ni utekelezaji wa azimio la Bunge katika Ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili.
Hata hivyo, watendaji hao, walirejeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kwamba baada ya Nyalandu kukataa kumtambua, wajumbe walimuunga mkono wakisema nao hawamtambui kwa sababu hatua aliyochukuliwa ilitokana na uamuzi uliofikiwa na Kamati ya Operesheni Tokomeza, ambayo ni sehemu ya Kamati hiyo ya Bunge.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Nyalandu alikiri kumzuia Songorwa kujitambulisha: “Kwanza sikujua kama angekuwapo katika kikao kile, maana suala lake bado hatujalizungumza ofisini. Sikuona sababu ya yeye kujitambulisha. Tukirejea ofisini tutalizungumza na kazi zitaendelea kama kawaida, ila azimio la Bunge dhidi yake lipo wazi. Uamuzi haurudi nyuma na itabidi apangiwe kazi nyingine.”
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembeli alishindwa kukiri wala kukataa kutokea kwa jambo hilo zaidi ya kusema jambo hilo iulizwe Wizara ya Maliasili na Utalii.
Profesa Songorwa hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu.

Thursday, May 1, 2014

Man arrested with 20 jumbo tails valued at 485 million/-



By The guardian reporter
29th April 2014

http://www.ippmedia.com/images/frontend/headline_bullet.jpghttp://www.ippmedia.com/images/frontend/headline_bullet.jpg  Another nabbed with 35 elephant tusks worth over 451m/-


Police in Songea District have arrested a man with at least 20 elephant tails estimated to value up to USD300,000 (about 485m/-).

Ruvuma Regional Police Commander Akili Mpwapwa confirmed the report over the weekend saying police officers, working of a tip from the public, arrested the suspect, one Kiambwe Ndomondo (30) on April 21.

The resident of Masasi District in Mtwara Region was nabbed in possession of a black bag that contained the 20 elephant tails.

He was arrested at the Biasi area of Nakayaya Ward in Tunduru District on his way to Masasi and was then taken to Tunduru Police station where he is still being interrogated by the police.

This is the second large bust this month following the police in Mtwara arrest of Julius Abeid (32), a resident of Likula Village, Nanyumbu District in Mtwara Region who was found with 35 elephant tusks valued at 451,440,000/-.

Mtwara Regional Police Commander Zelothe Stephen told a news conference here that the suspect was arrested at his residence thanks to a tip off by the public.

Abeid is now being held at the Mtwara Regional police station awaiting legal action.

He commended wananchi for their support and corporation urging them to continue with the same spirit for the protection of the county’s wildlife resources.
Mtwara District game ranger Sikujua Mwakinga said: “If everyone was as patriotic as the villagers here are, poaching in this country would end once and for all.”  
SOURCE: THE GUARDIAN
More News

Waliosimamishwa kazi na Nyalandu warejeshwa

Mkurugenzi wa Wanyama Pori Tanzania Profesa Alexander Songorwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Thailand Shinawatra muda mfupi baada ya kushuka uwanja wa ndege wa Seronera-picha na Journo Tourism.

Na Ibrahim Yamola, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Mei1  2014 

Kwa ufupi
Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo zimeeleza kuwa watendaji wote waliokuwa wamesimamishwa kazi wamerejeshwa na katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi.
Dar es Salaam. Agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu la kuwasimamisha kazi vigogo wa Idara ya Wanyamapori kwa kwenda kinyume na maadili ya kazi limetenguliwa baada wakurugenzi hao kurejeshwa katika nyadhifa zao.
Februari mwaka huu, Waziri Nyalandu alimsimamisha mkurugenzi wa wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na mkurugenzi msaidizi wa matumizi endelevu ya wanyamapori, Jafari Kidegesho, ikiwa ni utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Bunge Desemba 22 mwaka jana, iliyotaka Serikali kuwawajibisha watendaji waliozembea kwenye Operesheni Tokomeza Ujangili.
Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo zimeeleza kuwa watendaji wote waliokuwa wamesimamishwa kazi wamerejeshwa na katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi.
Alipotafutwa kwa njia ya simu katibu mkuu huyo hakuonyesha ushirikiano baada ya kugundua anaongea na mwandishi badala yake alibaki kusema: “Halooo..halooo…halooo” na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi hakujibu.
Hata alivyoendelea kupigiwa simu aliamua kumpa mwanaume apokee simu hiyo ambaye naye aliendelee kusema hasikii ingawa alikuwa akisikika vyema.
Kwa upande wake Profesa Songorwa alipotafutwa ali thibitisha kwamba ni kweli yupo kazini.
Kwa upande wake Kidegesho alisema yuko Morogoro akiendelea na vipindi Chuo Kikuu cha cha SUA lakini amesikia taarifa hizo.


Ripoti: Wawindaji halali ndiyo wanaovuna tembo




Uchunguzi huo ulibaini kuwa vinasaba vya pembe hizo vilifanana, hivyo kujenga dhana kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiwinda katika hifadhi hiyo mara kwa mara katika utaratibu maalumu unaotambuliwa na Serikali.PICHA|MAKTABA 
Na Peter Elias, Mwananchi

Posted  Jumatano,Aprili30  2014  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Ripoti hiyo inafafanua kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), katika tani 11 za pembe za ndovu zilizokamatwa Taiwan, Japan na Hong Kong mwaka 2006, ilibainika kuwa pembe 1,500 zilitoka Tanzania (Selous).
Dar es Salaam. Ongezeko la kasi ya ujangili nchini limedaiwa kusababishwa na vitendo vya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na mfumo dhaifu wa usimamizi wa sheria katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kwa mujibu wa ripoti iliyopewa jina la Urasimishaji wa Ujangili wa Kitaalamu Afrika, tangu mwaka 2000 wizara hiyo imejikuta katika kashfa za rushwa na kusababisha mawaziri na watendaji wakuu kuvuliwa nyadhifa zao.
Katika ripoti hiyo, Taasisi ya Kimarekani ya Utunzaji Wanyamapori ya Born Free USA kwa ushirikiano na Shirika la Ripoti za Kichambuzi na Takwimu la C4ADS, imeeleza pia jinsi vikundi vya waasi barani Afrika wanavyoendesha shughuli za ujangili.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa mwezi huu nchini Kenya, inaitaja Tanzania kama kitovu cha kusafirisha pembe za ndovu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikishindana na ile ya Mombasa katika kutumia bandari kibiashara.
Kutoka mwaka 2008 mpaka 2013, inaelezwa zaidi ya tani 20 za pembe za ndovu ama zilikamatwa zikisafirishwa kuingia au kutolewa katika Jiji la Dar es Salaam, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya C4ADS.
Ripoti hiyo inafafanua kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), katika tani 11 za pembe za ndovu zilizokamatwa Taiwan, Japan na Hong Kong mwaka 2006, ilibainika kuwa pembe 1,500 zilitoka Tanzania (Selous).
Uchunguzi huo ulibaini kuwa vinasaba vya pembe hizo vilifanana, hivyo kujenga dhana kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiwinda katika hifadhi hiyo mara kwa mara katika utaratibu maalumu unaotambuliwa na Serikali.
“Kuna udhaifu mkubwa katika usimamizi wa uwindaji halali na wawindaji wenye vibali hawasimamiwi ipasavyo kufanya uwindaji kwa taratibu zilizowekwa kisheria. Hivyo hutumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya ujangili,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Serikali yakanusha
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Paul Sarakikya alikanusha madai hayo akisema siyo kweli kwamba wawindaji halali huachwa bila usimamizi, bali wana mifumo ya kusimamia shughuli hiyo.
“Sikubaliani na ripoti hiyo, tumeshaongea sana juu ya suala hili, Rais alishalizungumzia na waziri pia. Ufafanuzi ndio huo, hamna ukweli wowote katika ripoti hiyo,” alisisitiza Sarakikya.
Salakikya alisema idadi ya tembo nchini inazidi kuongezeka katika hifadhi tofauti na upungufu unaoelezwa katika ripoti hiyo.
Mkurugenzi huyo alihoji kuwa kama hakuna usimamizi madhubuti katika uwindaji halali, wamewezaje kusimamia uwindaji miaka yote mpaka idadi ya tembo inaongezeka, baada ya upungufu uliokuwepo miaka ya nyuma.
Wakati Sarakikya akisema tembo wanaongezeka, ripoti hiyo inaeleza kuwa idadi ya tembo katika hifadhi za Selous na Mikumi kwa mwaka 1976, ilikuwa ni 109,419 lakini kufikia mwaka 2009, idadi hiyo ilishuka hadi kufikia tembo 38,975.
Nchi zilizoathirika zaidi na ujangili barani Afrika, zinatajwa kuwa ni Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Cameroon, Msumbiji, Kenya, Zimbabwe na Tanzania ambayo pia inatajwa kuwa kitovu cha usafirishaji wa pembe za ndovu.
Idadi ya tembo waliosalia
Na kwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Frankfurt Zoological Society mwishoni mwa mwaka 2013, ripoti hiyo inaeleza kuwa ni tembo 13,084 wanaokadiriwa kusalia katika hifadhi, sawa na upungufu wa asilimia 66 katika kipindi cha miaka minne tangu 2009.
Hii imefafanuliwa kuwa zaidi ya tembo 25,000 waliuawa katika Hifadhi ya Selous ndani ya miaka minne pekee. Pia, ripoti hiyo inabainisha upungufu wa tembo katika hifadhi ya Ruaha-Rungwa kutoka tembo 35,461 mpaka tembo 20,090 sawa na upungufu wa asilimia 36.5 kuanzia mwaka 1990 mpaka sasa.