Friday, March 14, 2014

Bilionea Mmarekani akoleza vita dhidi ya ujangili



 

 

Rais Jakaya Kikwete, akipokea mfano wa helikopta kutoka kwa mtoto wa bilionea wa pili duniani, Warren Buffett, Howard ambaye familia yake kupitia Mfuko wa Warren Buffett Foundation watatoa helikopta moja itakayotumika kupambana na ujangili katika Pori la Akiba la Selous. Picha ya Wizara ya Maliasili na Utalii. 




Na Mpoki Bukuku, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Marchi14  2014  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Akikabidhi mfano wa helkopta kwa Rais Kikwete, Buffett alisema amevutiwa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili hususan wa tembo na faru.
Dar es Salaam. Familia ya bilionea namba mbili nchini Marekani, Warren Buffett imeunga mkono juhudi za kupambana na ujangili nchini kwa kuchangia helikopta moja.
Familia ya Warren Buffett imeamua kutoa msaada huo kupitia Mfuko wa Howard Buffett Foundation, baada ya kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali.
Helikopta hiyo itatumika kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba nchini.
Msaada huo ulikabidhiwa juzi kwa Rais Jakaya Kikwete na mtoto wa bilionea huyo, Howard Buffett, ambaye yuko nchini kwa mapumziko ya kitalii.
Akikabidhi mfano wa helkopta kwa Rais Kikwete, Buffett alisema amevutiwa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili hususan wa tembo na faru.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema wamepokea kwa furaha ufadhili huo, ambapo utahusisha mafunzo kwa marubani wawili nchini Marekani ama Afrika Kusini kutokana na matakwa ya wizara.
“Wametuambia pesa ipo tayari ila ni jukumu letu sisi kama Serikali kuchagua aina ya helikopta tunayoitaka. Itakuwa na uwezo wa kubeba watu sita na kwa sasa tunaangalia kama tuchukue Bell ama Ecopter, wataalamu wanashughulikia,” alisema.

Thursday, March 13, 2014

SIMBA KIWA FARAGHA

 Haya yote ndani ya hifadhi za Taifa yanapatikana
Faragha ya Simba

Wednesday, March 12, 2014

Anti-poaching campaign gets boost




By Gadiosa Lamtey
12th March 2014


They will be used to expand surveillance and security in Serengeti National Park, Selous and Maswa Game reserves.

The eleven vehicles are part of Euro 20 million (equivalent to 40bn/-) set aside to help Tanzania’s fight against poaching in the next five years.

Five of the vehicles will go to Tanzania National Parks (TANAPA) to be used in Serengeti National Parks, while six will go to the Wildlife Division, five of which will be used in Selous Game Reserve and one in Maswa Reserve.

Speaking during the hand-over ceremony President Kikwete said while poaching for meat and trophies is a long standing problem in the country, of late killing of elephants for their tusks has reached alarming proportions. 

“As you are all aware, the number of elephants in Selous and Ruaha dropped from 74,416 in 2009 to 33,084 in 2013 due to poaching activities … this is alarming,” he said.
He said the government has scaled up the anti-poaching campaign, and the results have so far been promising.

The President said through Operesheni Kipepeo and Operesheni Tokomeza and 
other interventions the government has uncovered 
criminal networks, arrested 2,085 poachers and their accomplices in the illegal ivory trade network. 

“We have confiscated 1,721 weapons and several caches of arms used by poachers.  It has been a hard-won success. We need to sustain the gain because the problem remains unsolved,” he stressed.

He said the threat posed by poaching and illegal ivory trade to the world heritage and the country’s economy is real. Tourism is an important sector which contributes 17 percent of Tanzania’s GDP and employs over 300,000 people.

He said the challenge posed by the sheer size of the wildlife area is compounded by the insufficient game and warden staff currently at 1,155 personnel, which is only 24 percent of the actual need.

 The low number of staff dictates that, one person patrols about 169 square kilometres compared to the required international standard of 25 square kilometres per person.

 He said the government is in the process of employing 949 wildlife management officers and will continue to do so every year until the gap is closed in the next three to four years.

“The donation we have received today is indeed timely.  It has come at a time of serious need.  Certainly, the challenge before us is daunting, but we have no other choice. We need to build the capacity of our wildlife division to be able to fight this war and win,” Kikwete said.

He said the anti-poaching campaign cannot be won by Tanzania and affected countries alone. “This is a global problem that requires a global response.  It requires joint efforts from within and outside the elephant range in the country, and within and across regions,” he stressed.

Africa Director of FZS Robert Muir said the handover of the vehicles symbolises the fruitful partnership between FZS and the ministry of Natural Resources and Tourism. 
He said recent collaboration has also included the aerial wildlife census of the Selous Ecosystem in October 2013. The results from the census raised concerns about a rapid decline in elephant numbers, calling for increased protection efforts through ongoing monitoring and evaluation.

“As rhino and elephants poaching numbers reach unprecedented levels we at FZS commit to continue support to Tanapa and the Wildlife Division in order to expand surveillance and security” he said.  

Natural Resources and Tourism Lazaro Nyalandu said the operation Tokomeza II will kickoff anytime from now.He cautioned people who feed their animals in the national parks and game reserves to immediately stop because once the operation Tokomeza II starts it will not spare them.
SOURCE: THE GUARDIAN
More News

Rais Kikwete apokea magari ya kupambana na ujangili
Na Samson Fridolin
12th March 2014

Rais Jakaya Kikwete amepokea msaada wa magari 11 kwa ajili ya mpango wa kupambana na ujangili kutoka Taasisi ya Frankfurt Zoological Society (FZS) ya Ujerumani.

Akipokea magari hayo Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema serikali itaendelea kupambana na majangili ili kuhakikisha wanyama ambao wapo hatarini kutoweka wanaendelea kuwapo.

Alisema serikali inatambua kuwa tatizo la ujangili nchini ni kubwa na ndiyo maana ikiendesha operesheni maalumu mbalimbali ili kukomesha tatizo hilo pamoja na kuwapo na changamoto nyingi.

“Tunataka tuendelee na vita hii ndiyo maana tukawaomba wenzetu wa watusaidie vifaa ili jambo hili liwe endelevu kuwalinda wanyama hawa, tunahitaji vifaa vya kisasa pamoja na fedha ili kukabiliana ipasavyo na wanaoendesha ujangili nchini,” alisema Rais Kikwete.

Alisema katika bajeti iliyopita aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuajiri zaidi ya wafanyakazi 400 na katika bajeti inayokuja inatarajiwa kuajiri wafanyakazi 500 ili kuiongeza nguvu kazi katika mapambano hayo.


Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa Afrika wa Frankfurt Zoological Society, Robert Muur alisema magari hayo aina ya Land Rovers ni sehemu ya msaada wa Euro milioni 20 ambao ni mpango wa serikali ya Ujerumani katika kusaidia mapambano hayo.

Alifafanua kuwa, magari matano itapewa Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (Tanapa) ambayo yatapelekwa kwenye  Hifadhi ya Serengeti, matano yatapelekwa kwenye Hifadhi ya Selous , na moja litapelekwa Maswa kwa ajili ya mpango huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa masaada huo na kueleza kuwa inatia faraja kuona kuwa kuna wenzao ambao wanajitolea kutoa misaada kama hiyo kwani imekuja kwa wakati muafaka.

Alisema Tanapa itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wafadhili ili kuhakikisha kuwa ujangili unatoweka kabisa nchini ili wanyama waendelee kuwapo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
CHANZO: NIPASHE
Habari Zaidi



JK atangaza kiama cha majangili





Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imenuia kumaliza kabisa ujangili nchini, ikiwa ni hatua ya kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.
Hakusita kusisitiza kwamba, nia ya dhati ya Serikali ni kuhakikisha mkakati huo unakamilika, japokuwa kumekuwa na changamoto zinazotokana na ukubwa wa hifadhi hizo na uhaba wa vitendea kazi pamoja na askari wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa kupokea magari 11 ya kisasa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili kutoka kwa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la Ujerumani, Kikwete alisema tatizo hilo limekuwa la muda mrefu, lakini juhudi za kulikomesha zinafanyika.
Alisema, pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna tatizo la uhaba mkubwa wa wafanyakazi wanaotakiwa kudhibiti majangili, ambapo kwa sasa kuna wafanyakazi 1,155 sawa na asilimia 24 tu ya mahitaji halisi ya wafanyakazi 4,000 wanaohitajika.
“Mwaka uliopita, Serikali ilisimamia ajira ya wafanyakazi 449 na sasa kuna ajira ya wafanyakazi 500.
Kwa maana hiyo tutafikisha wafanyakazi wapya 949 na kufanya mahitaji ya wafanyakazi wapya kuwa 4,000 zaidi ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu kwa viwango vya kimataifa,” alisema.
Kwa mujibu wa viwango vilivyopo sasa, mfanyakazi mmoja anasimamia eneo la kilometa za mraba 169 ikilinganishwa na viwango vya kimataifa vya kilometa za mraba 25 kwa kila mfanyakazi mmoja.
Rais Kikwete alisema kwa sasa Serikali itaendelea kuajiri idadi hiyo ya wafanyakazi kila mwaka kwa miaka mitatu ijayo ili kuhakikisha pengo lililopo linazibwa.
Alisisitiza kuwa, kampeni dhidi ya ujangili ni suala la kimataifa na Tanzania au nchi zilizoathirika hazitaweza kulikabili bila ushirikiano wa kimataifa.
Alisema upo ulazima wa kuteketeza mitandao yote ya ujangili na kuwawajibisha ipasavyo watakaonaswa, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kulinda urithi huo wa dunia.
Ukosefu wa vifaa
Akifafanua, Rais Kikwete alisema kuongeza idadi hiyo ya wafanyakazi pekee haitakuwa na maana iwapo hawatakuwa na vifaa maalumu vya kisasa vitakavyowawezesha kukabiliana ipasavyo na tishio la ujangili.
Katika mkakati wa maboresho hayo, Kikwete alisema wanafanya jitihada za kuongeza idadi ya magari, kuongeza vifaa vya kisasa kwa ajili ya doria na vifaa vya mawasiliano, ambavyo vinahitaji uwezo mkubwa wa kifedha ambao utaweza kutekelezwa na serikali kwa kipindi kirefu iwapo haitapata msaada wa uwezeshaji kutoka kwa wadau.
Msimamo wa Wizara
Akizungumzia msimamo na mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Waziri Lazaro Nyalandu alisema kutokana na ukubwa wa tatizo, wanahitaji vifaa vya kisasa zaidi, ikiwamo helikopta na ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kufanya doria kwenye maeneo yote ya mbuga na hifadhi za taifa.
Aliwatahadharisha wafugaji wanaopenda kuingiza mifugo yao kwenye maeneo ya hifadhi, akiwataka kuondoa mifugo yao mapema kwa kuwa katika operesheni hiyo hakuna atakayeachwa.
“Katika operesheni hii, hakuna jangili wala mfugaji atakayeachwa iwapo atakutwa kwenye maeneo ya hifadhi,” alisema.
Alifafanua kwamba, msaada huo wa magari utapelekwa maeneo tofauti, matano kanda nane za Selous, mengine matano Hifadhi ya Serengeti na moja Hifadhi ya Maswa.
Mwaliko wa vyombo vya habari
Nyalandu alisema Wizara yake imevialika vyombo vyote vya habari vya kimataifa kwa ajili ya kuja kupata taarifa sahihi kuhusu kampeni dhidi ya ujangili zinavyotekelezwa ili kuepuka ripoti za upande mmoja kwa ajili ya kuweka usawa.
Alisema hatua hiyo ilichukuliwa na wizara yake walipokwenda kwenye mkutano maalumu na Rais Kikwete ulioandaliwa na mtoto wa Mfalme wa Uingereza, Prince Charles kwa ajili ya kuangalia namna ya kulinda wanyama walio hatarini kutoweka duniani, wakiwemo tembo na faru.