Wednesday, July 1, 2015
USIKU WA TUZO ZA UANDISHI WA HABARI ZA UTALII NA UHIFADHI
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiendelea na burudani mbalimbali kabla ya zoezi la utoaji wa tuzo halijaanza ,ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza. |
Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi akisalimiana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi Mrisho Salakikya ambaye alipewa tuzo maalum kutokana na kufanya utalii wa kupanda mlima Kilimanjaro kwa mara nyingi zaidi
Baadhi ya maafisa wa Tanapa na familia zao wakifuatilia mambo yanavyoendelea.
Maandalizi ya Tuzo yanaendelea kama inavyoonekana hapo.
Danie Mjema toka Mwananchi Kilimanjaro akipokea hundi ya sh 1 milioni ,cheti baada ya kuibuka mshindi wa tatu tuzo ya uhifadhi
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akimpongeza
Waziri wa Maliasili na Utalii Nyalandu akimkabidhi hundi ya 1.5 milioni Mussa Juma toka Mwananchi Arusha aliyeshika nafasi ya pili tuzo ya uhifadhi.
Hongera sana Mussa
Pokea hundi na cheti chako ,kwa kazi yako iliyotukuka ,anasisitiza Waziri
Waziri wa Maliasili na Utalii Nyalandu akimpongeza Anthony Mayunga Mwandishi wa habari kampuni ya Mwananchi Mkoa wa Mara baada ya kushika nafasi ya kwanza katika tuzo ya uhifadhi,kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi,katikati ni Katibu Mkuu wizara ya Malisili na Utalii na Mkurugenzi Bodi ya Utalii.
Hongera sana na pokea hundi ya 2 milioni,cheti,ngao na safari ya mafunzo katika moja ya nchi za Sadc,ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi wakati wa kukabidhi tuzo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Nyalandu akisaidiana na Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa kukabidhi hundi,ngao na cheti.
Tunataumbua mchango wako kwenye uhifadhi wanasisitiza
Kwa kweli nimekukubali anasisitiza waziri.
Jimmy Mengere wa Channel Ten akipokea tuzo yake.
Hongera sana
Maarufu kama Mayunga wa Redio Saut akipokea tuzo
Hongera sana
Kasilida Mlimila wa Staa Tv akipokea zawadi
Kagunamo toka Itv Mbeya akipokea zawadi
Magessa Magessa akipokea zawadi baada ya kuibuka mshindi wa tatu kwa kazi aliyotuma akiwa star tv kwa sasa yuko Acacia Gold Mine
Hongera sana Magessa
hongera Kasilda kwa kushinda tuzo mbili
Phinias Bashaya mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Kagera akipokea zawadi baada ya kushika nafasi ya pili tuzo ya utalii wa ndani
Subscribe to:
Posts (Atom)