Thursday, July 31, 2014

MAMBO YA UTALII

 Watalii wakiwa wamejipumzisha ,huku wakipata upepo mwanana
 Wanapeana story,hifadhi ya Taifa ya Serengeti hakuna kama hiyo duniani
Tukitoka hapa tunakwenda hivi,wanasoma ramani

UTALII UNAZIDI KUSHAMIRI HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

WATALII WAKIWA WAMEPUMZIKA
 LANGO LA NABI HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI WAGENI WAKIWA KATIKA PILIKAPILIKA MBALIMBALI

 WANASOMA RAMANI ILI WAJUE WANAKOTOKA,WALIKO NA WANAKOKWENDA
 NDEGE HAWA NI RAFIKI WA BINADAMU
WANAPENDEZA

Saturday, July 26, 2014

MAONESHO YA SERENGETI CULTURAL FESTIVAL YALIVYOFANA


BANDALA TBL LILILOSHEHENI KILA BIDHAA WAZIZALISHAZO LILIKUWA KIVUTIO KWENYE MAONESHO YA UTALII WA KITAMADUNI (SERENGETI CULTURAL FESTIVAL)HASA KINYWAJI CHAO CHA NDOVU KAMA SEHEMU YA KAMPENI DHIDI YA UJANGILI WA NDOVU

 NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MAHAMOD MUGIMWA AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA EMAKULATA MNIKO JINSI YA KUTENGENEZA VIATU VYA ASILI,WAKATI WA MAONESHO YA SERENGETI CULTURAL FESTIVAVL
 WASHABIKI WA YANGA NA SIMBA WALIPATA ZAWADI KUTOKA BANDA LA TBL.
VIFAA VYA KITAMADUNI HUPATIKANA HAPA,NI KAULI YA MMOJA WA WAJASILIRIAMALI WA KIUNDI CHA TWIMANYE,KINACHOTENGENEZA VITU VYA KITAMADUNI

Friday, July 25, 2014

SERENGETI CULTURAL CENTRE

BAADHI YA WANYAMA HUABUDIWA NA MAKABILA YA MKOA WA MARA
MOJA YA NYUMBA ZA ASILI ZILIZOKO SERENGETI CULTURAL CENTRE

TAMASHA LA UTALII WA KITAMADUNI

WATOTO WAKISHANGAA NGAMIA WAKATI WA SERENGETI CULTURAL FESTIVAL

Saturday, July 12, 2014

UTALII WA NDANI KWA KUTUMIA NGAMIA WAZINDULIWA MUGUMU-SERENGETI

NGAMIA AKIANDALIWA KWA AJILI YA KUBEBA MTU,
MTOTO AKIFANYA UTALII KWA KUTUMIA NGAMIA ,UTALII UNAOENDESHWA NA SERENGETI CULTURAL CENTRE
 NGAMIA HAO NI SERENGETI NA KILIMANJARO AMBAO WANATUMIKA KWA AJILI YA UTALII WA NDANI KATIKA KITUO CHA SERENGETI CULTURAL KATIKA ENEO LA MATARE KILOMETA 2.5 KUTOKA MJINI MUGUMU

Tuesday, July 1, 2014

WANASHERIA WA LHRC WAANZA KUTOA MSAADA WA KISHERIA BURE SERENGETI,

Wanasheria na wasaidizi wa sheria na haki za Binadamu wakiwa kazini



Juni 30,2014.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)kupitia mawakili na wanasheria wake kwa kushirikiana na Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu wilayani Serengeti Mkoa wa Mara wameanza wiki ya Msaada wa Kisheria bure kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Mwanasheria kutoka (LHRC )Rodrick Maro akiongea naWaandishi wa habari mjini  Mugumu alisema  lengo ni kutoa msaada wa Kisheria bure kwa jamii kuhusiana na masuala ya Kisheria,ushauri na kuwajengea uwezo Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu kuendelea kusaidia wananchi wasio na uwezo wa kupata mawakili.
Alisema kuwa wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya ambazo zimekuwa zikinufaika na huduma hiyo kutokana na kuwepo kwa wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu ,hivyo wanakuwepo kwa wiki nzima wakitoa huduma hiyo bure.
“Kuna matatizo mengi ya kisheria kwa wananchi hasa migogoro ya ardhi,ndoa ,mirathi,ukatili wa kijinsia  na inapotokea watu wanakosa haki zao huchukua uamzi usiostahili ….hivyo tunaona kuna  hitaji kubwa la msaada wa kisheria kwa jamii,”alisema
Mwenyekiti wa shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu wilayani Serengeti(WASHEHABISE)Samwel Mewama amesema huduma hiyo ambayo imekuwa ikitolewa kila mwaka imesaidia wananchi wengi kujua haki zao na kuzidai,njia ambayo inaimarisha msingi wa utawala bora.
Aidha Mewama amesema kuwa mwaka jana migogoro mingi ilihusu mirathi,ukatili wa kijinsia,migogoro ya ardhi na ndoa ilipata ufumbuzi na kuomba viongozi wahamasishe wananchi kujitokeza ili kupata ushauri utakao saidia kutatua migogoro ambayo mingine inachangiwa na watendaji wa serikali wasiojua hitaji la sheria.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Mugumu wamesema utaratibu huo ni mzuri na unawasaidia kwa kuwa watu wengi wanakosa haki zao kwa kutokujua sheria na hawana uwezo wa kulipia mawakili ili kuwawakilisha.
Jumla ya wilaya 28 zilizo na Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu hapa nchini zinatarajiwa kufikiwa na huduma hiyo.
Mwisho.

Wabunge waelezwa tishio la kutoweka tembo, faru



 Tembo hatarini kutoweka,picha na Journo Tourism
Na Jacqueline Massano
30th June 2014

Vitendo vya ujangili vinavyoendelea kukithiri nchini vinasababisha hatari ya kutoweka kwa wanyamapori nchini wakiwamo tembo na faru.

Profesa Davis Mwamfupe wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ametoa tahadhari hiyo bungeni mjini hapa wakati akitoa mada kwenye semina ya kuwajengea uelewa wabunge katika kulinda wanyamapori iliyoandaliwa na Chama cha Wabunge cha Kuhifadhi na Kulinda Wanyamapori.

Profesa Mwamfupe alisema kuwa hivi sasa, wanyama hao ambao walikuwa wengi katika mbuga na hifadhi mbalimbali nchini wamepungua kwa kiasi kikubwa na hivyo kuwa katika tishio la kutoweka.

Aliongeza kuwa hakuna takwimu zozote zinazoonyesha kuongezeka kwa wanyama hao bali zote zinaelezea kupungua kwa wanyama hao kutokana na vitendo vya ujangili uliokithiri nchini.

“Hali hii ndiyo iliyotupa mwamko wa kutoa elimu kuhusiana na hifadhi za wanyamapori na thamani ya wanyama hao.

Tumeona tukiwapa elimu ninyi waheshimiwa wabunge ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi, itakuwa ni rahisi kuwaelimisha wananchi katika maeneo yenu,” alisema.

Alisema njia mojawapo ya kukabiliana na janga hilo ni kuangalia namna ya kuwapa motisha na kuwatia moyo wale ambao wamekuwa wakitoa taarifa muhimu za siri kuhusiana na matukio ya ujangili nchini.
CHANZO: NIPASHE