Na Charles Kayoka, Mwananchi
Posted Alhamisi,Marchi27 2014 saa 13:59 PM
Kwa ufupi
Katika dunia ya utandawazi jamii
hushindwa kuuza utamaduni wao, na chakula na upishi vikiwa moja ya tamaduni
hizi.
Moja ya udhaifu mkubwa wa utangazaji
wa utalii ni kukosa ushirikishwaji wa sekta mbalimbali za uchumi wa nchi.
Kwa walio wengi utalii unafikiriwa
katika ufinyu wake wa kiasili wa kwenda mbuga za wanyama na kutembelea magofu
tu.
Ili utalii ukamilike, kuna vipengele
kadhaa ambavyo lazima viende sawa kama vile vivutio vyenyewe, usafiri na huduma
za utalii, malazi na chakula.
Ukiangalia blogu na tovuti nyingi
Tanzania utagundua kuwa zinatangaza vivutio vyenyewe tu, tena vile vya asili,
kwa ukubwa zaidi, lakini chakula hakionekani kama kuwa ni sehemu muhimu sana ya
utalii.
Licha ya kuwa watalii wengi kiasili
hutembelea mahali kutaka kuona, karibu wote hupendelea kujaribisha ladha mpya
ya vyakula na upishi wa asili katika maeneo wanayotembelea, na kwa hiyo ni
muhimu kuanza kufikiria uimarishaji wa utalii wa upishi.
Faida inakuwa kubwa sana. Kwanza
chakula ni kitu ambacho kila mgeni hulazimika kutumia, ingawa watu hawapendi
kuacha asili, lakini kwa vile utalii ni pamoja na kujaribu na kutenda ambayo
huna fursa nayo unakotoka, kula chakula na mapishi ya kigeni ni sehemu ya
furaha ya utalii.
Kwa kweli watalii wengi hutaka kujua
na kujaribu vyakula vya wenyeji wao, kwenda kwenye maeneo ambayo watapata
chakula cha kiasili, na pengine kujifunza kukipika wao wenyewe.
Kwa njia hiyo utalii unaweza
kutumika kutangaza chakula na mapishi ya nchi wanazokwenda, kiasi cha kuwezesha
kujenga mfumo wa mafunzo nje na ndani ya nchi.
Chakula ni utamaduni wa jamii.
Watalii kula na kujifunza mapishi ya wenyeji ni kuutangaza utamaduni, na njia
hiyo utalii wa chakula unaweza pia kuwa ni kuuuza utamaduni kwa wageni au nje
ya nchi.
Katika dunia ya utandawazi jamii
hushindwa kuuza utamaduni wao, na chakula na upishi vikiwa moja ya tamaduni
hizi. Tunapokula vitafunwa kama burger, sandwitch, hotdogs, cheese rolls,
croissants, na kadhalika, tunakuwa tunanunua utamaduni wa wageni, na
wanajipatia fedha nyingi kutokana na uuzaji huo kwani lazima watakuwa wanapata
mahitaji makubwa kutoka kwetu.
Kwa kuwa tunaununua utamaduni huo,
wanapata fedha za kuanzisha mafunzo, matangazo na hatimaye tunafikiria kuwa
kula vyakula vya huko ni bora zaidi.
Kumbe basi tukirahisisha na
kuboresha upishi na matangazo ya vyakula vyetu, tunaweza kutengeneza chanzo cha
mapato kwa wananchi wetu.
Nchi kadhaa duniani huwa na matukio
ya kitaifa yanayohusisha chakula na hatimaye yamekuwa ni vivutio vya utalii.
Hapa kwetu tumebuni matukio kama ya Siku ya Nyama Choma, Siku ya Vipapatio vya
Kuku, lakini hayako endelevu na hayaoanishwi na utalii.
Aidha matukio ya minada ya nyama
choma kama kule Arusha, Morogoro na Dodoma, bado hayajafikia ukubwa wa
kiutalii, hata hivyo tunaweza kuanzia hapo.
Waliotembelea nchi za Ulaya
watakubaliana na mimi kuwa matunda yaliyovunwa na kuuzwa kwa kutoka shambani
moja kwa moja huwa ni bidhaa ghali sana, na wageni wanapokuja hapa kwa kweli
matunda huwa ni moja ya vyakula wanavyopenda kununua kwa sababu yametoka
shamba.
Uchambuzi
Hivi kweli Serikali haiwezi kupambana na majangili?
Na Boniface Meena
Posted Alhamisi,Marchi27 2014 saa 13:18 PM
Kwa ufupi
Haiwezekani majangili wakaua hata
wale vifaru ambao Rais Kikwete aliwapata Afrika Kusini na kuwawekea ulinzi,
halafu tukasema majangili ni watu wa kawaida.
Tuna vita mikononi mwetu hivyo ni
muhimu tutumie kila tulichonacho kupambana na kushinda vita hiyo.
Vita hiyo ni ujangili ambao
umekithiri nchini Tanzania, ambako vitisho vingi vimetolewa na viongozi wa
ngazi mbalimbali za Serikali, lakini ujangili bado unaendelea kukithiri.
Majangili ni watu wa aina gani au ni
maroboti? Ni lazima tuanze kujiuliza kwa kuwa haiwezekani wakawa binadamu wa
kawaida ambao wanaweza kuishinda nguvu ya Serikali ambayo ina kila kitu cha
kuweza kupambana nao.
Ripoti ya Shirika la Polisi la
Kimataifa (Interpol) iliyotolewa hivi karibuni inaeleza kuwa mwaka jana
Tanzania ndiyo ilikuwa kinara au kitovu cha biashara ya meno ya tembo katika
nchi za Afrika Mashariki.
Imeeleza kuwa takribani tembo 30
huuawa kila siku nchini na kufanya tembo 10,000 kuuawa kwa mwaka. Yaani tembo
30 huuawa kila siku na Serikali imekaa kimya ikipiga kelele kuwa itapambana na
majangili kwa njia yoyote ile ili kukomesha tatizo hilo.
Serikali ina jeshi, ina polisi ina
usalama wa taifa bado tembo 30 wanauawa kila siku na majangili ambao
wamejengewa dhana kuwa wanaizidi “nguvu Serikali” na kufanya mauaji ya tembo na
vifaru wakati wowote ule wanaojisikia.
Kwa jinsi hali ilivyo na
inavyoendelea, inatia wasiwasi kuwa huenda majangili hao ni viongozi walioko
Serikalini ambao hawawezi kudhibitiwa kwa njia yoyote ile au ndio wanaowalinda
majangili kwa masilahi yao binafsi na familia zao. Nasema hivyo kwa kuwa ni
aibu kwa Serikali kwenda kupiga domo Ulaya kuwa inapambana na ujangili nchini
kwa nguvu zake zote, halafu tembo 30 wakawa wanaendelea kuuawa kila siku.
Haiwezekani majangili wakaua hata
wale vifaru ambao Rais Kikwete aliwapata Afrika Kusini na kuwawekea ulinzi,
halafu tukasema majangili ni watu wa kawaida.
Hapana! Hawa watu ni lazima watakuwa
na mizizi mikubwa serikalini na kwenye vyombo vya usalama kiasi cha kuamua
kufanya chochote, wakati wowote katika mbuga zetu za wanyama halafu kazi ya
Serikali au wasimamizi wa mbuga iwe ni kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa
majangili wameua tembo na kutoroka na meno yake.
Lazima kuna mkono wa mtu na ndiyo
maana Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mabadiliko ya wakurugenzi hadi
mawaziri, lakini bado ujangili unaendelea kukua kwa kasi badala ya kupungua.
Idadi ya tembo nchini imeendelea
kupungua miaka ya karibuni hasa katika pori la akiba la Selous ambalo lilikuwa
na kiasi cha tembo 70,000 mwaka 2006, lakini idadi hiyo imeendelea kupungua
hadi tembo 39,000 mwaka 2009 na hivi sasa pori hilo linao tembo 13,084.
Iadi ya tembo katika mbuga ya Ruaha
nako imepungua kwa asilimia 44 toka 2006 na hivi sasa inakadiriwa ina tembo 20,
090.
Tuna vita mikononi mwetu hivyo ni muhimu tutumie kila tulichonacho kupambana
na kushinda vita hiyo.
Vita hiyo ni ujangili ambao umekithiri nchini Tanzania, ambako vitisho vingi
vimetolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali za Serikali, lakini ujangili bado
unaendelea kukithiri.
Majangili ni watu wa aina gani au ni maroboti? Ni lazima tuanze kujiuliza
kwa kuwa haiwezekani wakawa binadamu wa kawaida ambao wanaweza kuishinda nguvu
ya Serikali ambayo ina kila kitu cha kuweza kupambana nao.
Ripoti ya Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) iliyotolewa hivi
karibuni inaeleza kuwa mwaka jana Tanzania ndiyo ilikuwa kinara au kitovu cha
biashara ya meno ya tembo katika nchi za Afrika Mashariki.
Imeeleza kuwa takribani tembo 30 huuawa kila siku nchini na kufanya tembo
10,000 kuuawa kwa mwaka. Yaani tembo 30 huuawa kila siku na Serikali imekaa
kimya ikipiga kelele kuwa itapambana na majangili kwa njia yoyote ile ili
kukomesha tatizo hilo.
Serikali ina jeshi, ina polisi ina usalama wa taifa bado tembo 30 wanauawa
kila siku na majangili ambao wamejengewa dhana kuwa wanaizidi “nguvu Serikali”
na kufanya mauaji ya tembo na vifaru wakati wowote ule wanaojisikia.
Kwa jinsi hali ilivyo na inavyoendelea, inatia wasiwasi kuwa huenda
majangili hao ni viongozi walioko Serikalini ambao hawawezi kudhibitiwa kwa
njia yoyote ile au ndio wanaowalinda majangili kwa masilahi yao binafsi na
familia zao. Nasema hivyo kwa kuwa ni aibu kwa Serikali kwenda kupiga domo Ulaya
kuwa inapambana na ujangili nchini kwa nguvu zake zote, halafu tembo 30 wakawa
wanaendelea kuuawa kila siku.
Haiwezekani majangili wakaua hata wale vifaru ambao Rais Kikwete aliwapata
Afrika Kusini na kuwawekea ulinzi, halafu tukasema majangili ni watu wa
kawaida.
Hapana! Hawa watu ni lazima watakuwa na mizizi mikubwa serikalini na kwenye
vyombo vya usalama kiasi cha kuamua kufanya chochote, wakati wowote katika
mbuga zetu za wanyama halafu kazi ya Serikali au wasimamizi wa mbuga iwe ni
kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa majangili wameua tembo na kutoroka na
meno yake.
Lazima kuna mkono wa mtu na ndiyo maana Wizara ya Maliasili na Utalii
imefanya mabadiliko ya wakurugenzi hadi mawaziri, lakini bado ujangili
unaendelea kukua kwa kasi badala ya kupungua.
Idadi ya tembo nchini imeendelea kupungua miaka ya karibuni hasa katika pori
la akiba la Selous ambalo lilikuwa na kiasi cha tembo 70,000 mwaka 2006, lakini
idadi hiyo imeendelea kupungua hadi tembo 39,000 mwaka 2009 na hivi sasa pori
hilo linao tembo 13,084.
Iadi ya tembo katika mbuga ya Ruaha nako imepungua kwa asilimia 44 toka 2006
na hivi sasa inakadiriwa ina tembo 20, 090.