Monday, February 17, 2014

Meno ya tembo kilo 130 yanaswa




http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1596856/data/43/-/appotyz/-/ico_plus.png 

Meno ya Tembo yanayosakwa na wafanyabiashara wakubwa huku soko lake likitajwa kuwa nchini China. Picha na Maktaba 
Na Waandishi wetu, Mwananchi

Posted  Jumapili,Februari16  2014  saa 3:0 AM
Kwa ufupi
Yalikuwa yakisafirishwa na watuhumiwa watatu kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.


Singida/Mtwara. Ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kukiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu linaloielemea Tanzania, Jeshi la Polisi mkoani Mtwara na Singida linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha nyara za Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga alisema kuwa jeshi hilo limewakamata watu watatu wakiwa na meno ya tembo 58 yenye uzito wa kilogramu 130.6 yenye thamani ya Sh700.3 milioni.
Kamanda alieleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa saa 11:00 alfajiri katika Kijiji cha Chungu Kata ya Nanyumbu, Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakiwa katika kizuizi cha barabara ya Mtambaswala – Mangaka wakielekea jijini Dar es Salaama.
“Tunawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali ambazo ni meno ya tembo 58 yenye uzito wa kilogramu 130.6 na thamani ya 700.3 milioni, ambapo ni sawa na tembo 29 waliouawa yakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser,” alisema Kamanda Manganga.
Alisema mbinu waliyotumia watuhumiwa hao ni kukata sakafu ya gari ya chini ya kiti cha nyuma ya dereva na kutengeneza tanki la bandia na kuweka meno hayo kisha kuweka kapeti juu yake.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamidu Ngunde (40) dereva, Geraldat Lukas (36) dereva na Boniphace Kosan (29) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam na kusema kuwa gari iliyotumika kusafirisha meno hayo ni mali ya Hilali Rashid.
Wakati huo huo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alisema wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, Februari 13 mwaka huu saa 2.30 asubuhi katika kizuizi cha Mazaoa ya Misitu na Chakula kilichopo katika Kijiji cha Ukimbu Kata ya Mgandu, tarafa ya Itigi, Wilaya ya Manyoni.
Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya Toyota lenye namba T.797 CQL kusafirisha nyara za Serikali kutoka Kijiji cha Mwamangembe kwenda Itigi Mjini.
“Nyara alizokamatwa nazo mtuhumiwa zilikuwa zimewekwa kwenye mabegi mbalimbali ya nguo,” alifafanua. Kamwela alisema uchunguzi wa awali, umeonyesha kuwa vipande hivyo 21 vinakadiriwa kuwa vya tembo wanne, vina uzito wa kilogramu 49 na thamani ya Sh43.1 milioni.

Kuvamiwa watalii kwatia doa Zanzibar


Na Herieth Makwetta, Mwananchi

Posted  Jumapili,Februari16  2014  saa 3:0 AM
Kwa ufupi
  • Akizungumza na Mwananchi Jumapili Mjini Zanzibar, Ferouz alisema mashambulizi hayo yalikuwa mabaya na yalichafua mfumo mzuri uliojengwa kwa kipindi kirefu katika visiwa hivyo, na kwamba yamerudisha nyuma juhudi za tume ya kukuza utalii ndani ya Visiwa vya Zanzibar.
  
Zanzibar. Katibu Mkuu wa Tume ya Utalii Zanzibar, Salehe Ramadhani Ferouz, amesema mashambulizi ya baadhi ya watalii waliowahi kutembelea visiwa vya Zanzibar, yameifanya picha ya kisiwa hicho cha amani kubadilika.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Mjini Zanzibar, Ferouz alisema mashambulizi hayo yalikuwa mabaya na yalichafua mfumo mzuri uliojengwa kwa kipindi kirefu katika visiwa hivyo, na kwamba yamerudisha nyuma juhudi za tume ya kukuza utalii ndani ya Visiwa vya Zanzibar.
“Kama tume, tuna wakati mgumu sana kwa sasa, japokuwa wageni katika tamasha hili la Sauti za Busara wamekuwa ni wengi, lakini tuna imani mwaka huu idadi ingekuwa kubwa zaidi, vitendo hivi ndivyo vinatukwamisha,” alisema.
Kwa mujibu wa ofisa huyo wa utalii wa Zanzibar, amesema kuwa wamekuwa wakikusanya wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani, tangu kuanzisha kwa tamasha hilo kwa mara ya kwanza miaka 11 iliyopita.
“Tunapata ahueni kubwa ya watalii wakati wa tamasha hili linalochukua muda wa siku nne, hoteli zote hapa mjini zimejaa, hii yote ni katika utalii wa muziki kwani wengi zaidi wanapendelea kuja msimu huu kushuhudia tamasha la muziki wa asili,” alisema Ferouz.
Kwa mujibu wa Ferouz, utalii ni sekta inayoongoza katika kukuza uchumi Zanzibar kwnai inachangia asiliamia 25 ya Pato la Taifa (GDP) na asilimia 80 ya ukusanyaji wa kodi za serikali.
Mwishoni mwa mwaka jana , Zanzibar ilikuwa inakabiliwa na mashambulizi ya tindikali, ambayo wanawake wawili kutoka Uingereza Katie Gee na Kirstie Trup, wote wakiwa na umri wa miaka 18, wakati wakitembea katika njia ya sehemu ya zamani ya mji mkuu wa Zanzibar, walimwagiwa tindikali na watu wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki.
Mashambulizi ya hivi karibuni yakiwamo ya upotevu wa wanandoa wa Kifaransa ambao wanaaminiwa kwamba waliuawa na kutupwa katika kisilinalozunguka nyumba yao.
Francois Cherer Robert Daniel na Brigette Mery walionekana kwa mara ya mwisho mwaka jana. Taarifa kwamba wamepotea zilianza kutangazwa Desemba 27 mwaka jana.


Govt defends Serengeti road


By Zephania Ubwani, The Citizen Bureau Chief

Posted  Sunday, February 16  2014 at  04:00
In Summary
  • Government Counsel Gabriel Malata told the East African Court of Justice that the highway would ease the movement of tourists to and from the area.

Arusha. The government has defended the proposed highway across the Serengeti National Park, saying constructing it will neither violate the East African Community (EAC) Treaty nor harm the ecosystem.
Government Counsel Gabriel Malata told the East African Court of Justice that the highway would ease the movement of tourists to and from the area.
When the case was filed in December 2010, he explained, the government had not decided on whether to build a tarmac or gravel road. After a feasibility study, Mr Malata said, the gravel road came out on top--essentially because it would have no effect on the Serengeti eco-system.
Mr Malata, the principal state attorney, asked the court to dismiss the case filed by the Nairobi-based Africa Network of Animal Welfare (ANAW) with costs. He argued that supporting ANAW would frustrate the tourism sector in the entire region “because the road is there to facilitate the movement of tourists”.
The EAC partner states were yet to ratify the Protocol on Environment and Natural Resources, he added, making the case premature.
ANAW argues that construction of the road will be hazardous to the environment and animals in particular. The group’s lawyer, Saitabao Kanchory Mbalelo told the court that construction of the road across the national park infringes Articles 5 and 3 of the EAC Treaty.


London wildlife summit moves to choke off ivory markets

Posted  Saturday, February 15  2014 at  10:00
In Summary
  • The London Declaration urges practical steps to end the illegal trade in rhino horn, tiger parts and elephant tusks that contribute to criminal activity worth more than $19 billion (14 billion euros) each year.

Related Stories
London. More than 40 countries including China and African states have signed a declaration aimed at stamping out the illegal trade in wildlife, in a move broadly welcomed by conservation groups.
The London Declaration urges practical steps to end the illegal trade in rhino horn, tiger parts and elephant tusks that contribute to criminal activity worth more than $19 billion (14 billion euros) each year.
British Foreign Secretary William Hague, who hosted Thursday’s meeting, said: “I believe the measures we have agreed can mark a crucial turning point.”
Hague highlighted the attendance of China and Vietnam, two major consumers of the banned products. Beijing sent Forestry Vice minister Zhang Jianlong.
“I do welcome the involvement of China (and) the constructive approach from their minister and from other Asian countries, but there will be more work to do,” Hague said. He highlighted the progress that China had made in reducing the number of sharks killed to make shark fin soup, a traditional Chinese delicacy.
“The conference wants to follow this example in other areas,” he said. Conservation groups gave the declaration a largely positive reception, but said it did not go far enough.
Ms Mary Rice of the London-based Environmental Investigation Agency said: “This has been an unprecedented gathering, the first indication that many of the world’s governments are really serious about combating organised wildlife crime.
“We would have liked them to go further and, specifically with regard to ivory and tigers, close down legal domestic markets.”
Tanzania, Chad, Gabon, Ethiopia and Botswana announced a separate action plan to protect elephants of which 25,000 are killed each year by poachers, according to official estimates.
Botswana will organise a conference in 2015 to evaluate progress on the initiative.
Opening the meeting, British heir to the throne Prince Charles , said that while it was important to tackle poachers, the key thing was to “attack demand” for rare creatures which are used to produce traditional medicines and other products.
Charles said the declaration would “address what is the most significant problem in my view -- that of demand for and consumption of specific products from critically endangered wildlife. Most recently, demand from Asia -- particularly China -- has fuelled the trade, but we also know that the US and Europe are contributing to it.”
While estimates of the value of the illegal trade in wildlife vary -- London’s Chatham House think-tank puts it at $10 billion -- all the participants agree that poaching is accelerating at an alarming rate. (AFP)
The conference heard that 1,000 rhinos were killed in South Africa last year compared with just 13 in 2007, and the number of tigers living wild in Asia has plunged from 100,000 to just 3,200 in the space of 10 years.
Martial arts film star Jackie Chan attended the conference to call for urgent action. He told AFP: “I don’t want my grandchildren to look in a book and say ‘what is that, rhino?’.
“We have already destroyed the earth enoughl

Wabunge watahadharisha ujangili kudhoofisha uchumi

Na Mwandishi maalum
15th February 2014

Wakati sakata la mtandao wa ujangili nchini likiendelea kutikisa, umoja wa wabunge wa kusimamia hifadhi ya Wanyamapori, umetoa tahadhari kwa Watanzania kuchukua tahadhari za mapema kwa kundi linalojihusisha na vitendo hivyo kwa sababu linaweza kuua uchumi wa taifa.

Sambamba na hilo, umetoa angalizo kwa serikali juu ya mikataba inayoingia na nchi za jirani hususani zile zinazohusika na ujenzi wa barabara kwasababu wimbi hilo linatumia mwanya huo kama sehemu mahususi ya biashara yao.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Umoja huo, ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Riziki Lulida, alisema ongezeko la wageni nchini, ambao wanaishi muda mrefu bila sababu maalumu limechangia kwa kasi kupotea au kuuawa kwa wanyamapori.

“Suala la kusimamia ujangili ni letu sote hivyo tuache malumbano pasipo sababu, tushikamane kwa pamoja kwa sababu hali ni tete ukilinganisha kundi hili limebebwa na watu wakubwa wanaotumia njia mbalimbali za kuangamiza rasilimali ya nchi.”

Alitoa mfano kuwa "awali tulishtushwa na taarifa za kuuliwa kwa wanyamapori sehemu za Kilindi mkoani Lindi, ambapo tulikutana na uongozi wa kijiji, lakini wahusika walidai hali ngumu ya maisha imechangia kuua wanyamapori hao” alisema Riziki.

Kwa upande wake mbunge wa Dole Zanzibar, Sylivester Mabumba (CCM), alisema miaka 10 ya nyuma taifa lilikuwa na idadi ya wanyamapori wengi ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya, Burundi, Rwanda, China, lakini kwa sasa wageni hao wameligeukia taifa.

Naye mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), alisema, umoja huo umesikitishwa na kauli ya mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa, juu ya Rais Jakaya Kikwete kuhusika na hujuma za ujangili huo, badala yake umesema kama ni pungufu ni wakawaida kwa kila kiongozi.

“Siasa iwe na mipaka yake jamani, kwanza tuna wasiwasi na kauli aliyoitoa Mchungaji Msigwa kwa sababu inaweza kuleta madhara makubwa ndani na nje ya nchi siku za usoni” alisisitiza Beatrice.

 

CHANZO: NIPASHE
Sunday Feb 16, 2014


http://www.ippmedia.com/images/frontend/headline_bullet.jpg  Atoboa baada ya kutinga CNN, BBC
http://www.ippmedia.com/images/frontend/headline_bullet.jpg  Wamo vigogo 40, baba lao liko Arusha

Rais Jakaya Kikwete, amesema mtandao wa majangili unajulikana na jitihada za serikali zimefanikiwa kukamata vigogo 40 walio kwenye mtandao mkubwa wa biashara ya nyara hizo za serikali.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC , jana asubuhi alisema watuhumiwa hao wamebainika kuwa wanajihusisha na mtandao kwenye ukanda wa Kaskazini na kwamba tajiri mkuu wa biashara hiyo naye amefahamika na kwamba anapatikana mkoani Arusha .

Akizungumza katika kipindi cha Amka na BBC , alikozungumzia ujangili, alieleza kuwa mtandao umefahamika na kwamba unahusisha matajiri na miongoni mwa watu hao 40 yupo tajiri huyo wa Arusha ambaye hakutaka kumtaja jina redioni.

“Tumeutambua mtandao huo hadi wakubwa zao ni matajari pale Arusha kuna mmoja mkubwa ambaye sitaki kumtaja jina alikuwa akiendesha biashara hiyo naye yupo kwenye kundi hili la watu 40 kazi iliyokuwa ikifanyika ni kuutambua huo mtandao kwa upana,” alisema.

Awali alisema Tanzania ilikuwa na tembo wengi barani Afrika na hata duniani wakati huo baada ya Uhuru walikuwa 350,000 na ilipofikia mwaka 1987 walipungua hadi 55,000.

Alisema hapo ndipo serikali ilipofanya maamuzi ya kuingiza jeshi katika mapambano ya kupambana na ujangili jambo lililosaidia kwa kiasi kupunguza tatizo.

Hata hivyo, alisema ilipofikia mwaka 1989 shirika linaloshughulikia haki za wanyama walioko hatarini kutoweka (CITES) ilifanya maamuzi ya kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu duniani.

Rais Kikwete alisema kwa mambo hayo mawili ikiwamo nguvu ya jeshi kuingilia kupambana na ujangili pamoja na biashara hiyo kupigwa marufuku duniani ilisaidia kupungua ujangili na tembo kuanza kuonekana.

Alisema ilipofika mwaka 2009 hesabu ilikuwa kubwa ambapo idadi ya tembo iliongezeka na kufikia 110,000.

Alipohojiwa juu ya gazeti moja la Uingereza la Daily Maili kumuandika kuwa hajafanya jitihada za kutosha kupambana na ujangili, alisema gazeti hilo limeandika uongo na kwamba serikali imejitahidi kufanya mikakati mbalimbali kuokoa maisha ya tembo na kupunguza ujangili.

Pembe hizo za ndovu wanaouliwa Afrika soko lake lipo katika nchi za Asia ikiwamo China.

Kikwete alisema jitihada mbalimbali zimefanywa ndiyo maana mtandao huo ambao unajihusisha na biashara ya meno ya tembo umegundulika.

Wakati Rais akiwa kwenye mkutano nchini Uingereza uliokuwa ukijadili ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na pembe za faru, polisi mkoani Singida wamemkamata George James na vipande 21 vya meno hayo.

Polisi ilisema meno hayo yenye thamani ya Sh. milioni 43 yana uzito wa kilo 49.

MAHOJIANO NA CNN

Wakati huo huo, ujangili umemfikisha Rais Kikwete, kwenye televisheni ya CNN ya Marekani, alikohojiwa akitakiwa kueleza vita dhidi ya majangili inayofanyika nchini.

Akihojiwa na CNN jijini London juzi, alisema Tanzania imefanya operesheni nyingi dhidi ya majangili na kuhimiza haja ya mataifa makubwa kusaidia juhudi za kupambana na ujangili huo.

Akijibu maswali ya Christiane Amanpour wa CNN, Rais alitaka dunia kuungana kusimamisha biashara ya pembe za ndovu.

Alieleza kuwa hatua hiyo itaondoa kichocheo cha mtu kuwaua wanyama hao
Alieleza kuwa wakati wa uhuru walikuwepo tembo 350,000 kabla ya kuibuka wimbi la ujangili mkubwa ulioiachia nchi tembo 13,000 pekee.

AHADI YA MSAADA
Akijibu swali kama kuna ahadi yoyote aliipata katika mkutano juu ya ulinzi wa wanyama pori uliofanyika London juzi, Rais Kikwete aliitaja Canada kuwa imeahidi kutoa Dola milioni mbili, wakati serikali ya Uingereza imeahidi kutoa msaada.

ALICHOTARAJIA
Alieleza kuwa kitu muhimu kwake na viongozi wa Afrika ni kufahamisha kuwa ili kuupiga vita ujangili kunahitajika rasilimali watu, kuwajengea uwezo askari wa wanyama pori wa kulinda wanyama.
Rais alisema alikuwa anategemea nchi zilizoendelea hasa Uingereza na Marekani kusaidia upande wa mafunzo ya askari wa wanyama pori na pia kuwapatia vifaa.
Alitaja silaha, magari na vyombo vyenye uwezo wa kufanya uchunguzi na kwamba ndicho alichotegemea kutoka kwenye mkutano huo na kwamba amepata ahadi za msaada.

AKIBA YA MENO
Rais Kikwete alisema Tanzania ina karibu tani 112 za pembe za ndovu ambazo haijajua itazifanya nini kwa sababu nchi ilizoea kuomba idhini ya kuziuza hatua ambayo inahitaji kuangaliwa upya.

UMASKINI
Akijibu swali kuhusu kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa kulinganisha na nchi nyingine katika kipindi cha miaka michache iliyopita lakini nchi ikiwa na maskini wanaoishi kwenye ufukara, alisema “uchumi unakua kwa asilimia 70 lakini umasikini unapungua kwa asilimia 2.0” akiongeza kuwa mchango huo wa ukuaji wa asilimia 7.0 umetokana na sekta ya mawasiliano na usafiri.

Sunday Feb 16, 2014


Kwa siku tatu mfululizo, yaani kuanzia Jumatatu hadi Jumatano (jana), gazeti hili lilichapisha taarifa ya uchunguzi kuhusu hali ya ujangili nchini, namna unavyofanyika na mianya inayochochea kushamiri kwake.

Wakati taarifa hiyo ikichapishwa, mambo kadhaa yalishajadiliwa kwenye jamii, huku shinikizo kubwa likielekezwa kwa serikali na mamlaka zake husika, kuwekeza zaidi katika mkakati utakaofanikisha ujangili dhidi ya rasilimali za taifa, hususani tembo, unakomeshwa.

Jamii haikulijadili tatizo hilo linalokua kwa kasi nchini kama sehemu ya malumbano ya kawaida, ama kuwa kielelezo cha chuki dhidi ya serikali iliyopo madarakani, la hasha.

Kuna kila viashiria vinavyoonyesha kuwa mijadala kuhusu kushamiri kwa ujangili nchini kulitokana na kiu ya umma, kutaka kushuhudia taifa likiudhibiti uovu huo, ili rasilimali zake zibaki kuwa endelevu, zikikinufaisha kizazi cha sasa na baadaye.

Ni kupitia mijadala inayohusu ujangili na namna ya kukabiliana nao, umma hautaki kuiona Tanzania ikipoteza rasilimali zake kama wanyamapori wakiwamo tembo walio katika hatari ya kutoweka, bali waendelee kuwapo.

Kuwapo kwa rasilimali hizo kutafuta uwezekano wa Watanzania kusafiri kwenda kuwaona nje ya nchi.

Hilo halitaepukwa ikiwa jitihada za kuudhibiti ujangili hazifanikiwa.

Ndiyo maana, kutokana na umuhimu huo, gazeti hili lilianzisha dawati maalum kwa ajili ya habari za uchunguzi.

Dawati hilo ndilo lililofanikisha kupatikana kwa taarifa na vielelezo mbalimbali vilivyofanikisha kuchapishwa kwa taarifa ya uchunguzi kuhusu hali ya ujangili na namna bora ya kuudhibiti, ili Tanzania iendelee kuwa mahali salama kwa wanyamapori. 

Yapo mambo mengi yaliyoainishwa katika habari hiyo, lakini moja ya misingi yake mikubwa ni hitaji la kuifanya vita dhidi ya ujangili imilikiwe na umma wa Watanzania.

Kuimilikisha vita hiyo kwa umma kuna maana moja kubwa, kwamba hatua zozote zinazohusu ulinzi na usalama wa wanyamapori, zinapaswa kujulikana na kuushirikisha umma hasa jamii zinazoishi maeneo yaliyo karibu na hifadhi na mbuga za taifa, mapori ya akiba na mapori tengefu.

Hatua hiyo haipaswi kufanyika katika ‘taswira ya kisiasa’ lakini uhalisia wake ukabaki kuwa kinyume chake.

Umma unaposhiriki vita dhidi ya ujangili, kwa maana nyingine ni kuifanya kuwa rafiki wa rasilimali hizo na kwamba sheria, kanuni na taratibu zilizopo visiwe mfano wa nyenzo za kujenga uadui kati ya wenye dhamana ya ulinzi na usalama wa rasilimali hizo kwa upande mmoja na umma kwa upande mwingine.

Umma una nafasi kubwa kwa maana ndiyo unaochangamana na majingili wanapofika kwenye maeneo husika ili kutimiza nia ovu dhidi ya rasilimali zetu.
 



Thursday, February 6, 2014

Operesheni hii ianze kwa kutaja wabunge majangili

Operesheni hii ianze kwa kutaja wabunge majangili


Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu. PICHA|MAKTABA 


Posted  Jumatano,Februari5  2014  saa 10:59 AM
Kwa ufupi
  • Ni vyema tukakiri hapa kwamba awamu ya pili ya operesheni hiyo inaonyesha dalili za mafanikio hata kabla haijaanza, kwani Serikali inaonekana imejizatiti ipasavyo kwa kuweka utaratibu wa kuratibu na kutekeleza operesheni hiyo ili kasoro zilizojitokeza katika awamu ya kwanza zisirudiwe,   pia kwa kuonyesha bayana kuelewa ukubwa wa tatizo na changamoto itakazopambana nazo wakati wa utekelezaji.Share


Serikali imetangaza rasmi kuanza upya kwa ‘Operesheni Tokomeza Majangili’, baada ya kuisitisha zaidi ya miezi mitatu iliyopita kutokana na operesheni hiyo kukumbwa  na matatizo ya utekelezaji, ambapo vilitokea vitendo vya ukatili na mateso na kuwaacha raia 13 na askari 6 wakiwa wamepoteza maisha. Matukio hayo ya kusikitisha yalisababisha mawaziri wanne kupoteza nyadhifa zao serikalini baada ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii iliyoundwa kuchunguza vitendo hivyo kuwasilisha taarifa yake bungeni.
Ni vyema tukakiri hapa kwamba awamu ya pili ya operesheni hiyo inaonyesha dalili za mafanikio hata kabla haijaanza, kwani Serikali inaonekana imejizatiti ipasavyo kwa kuweka utaratibu wa kuratibu na kutekeleza operesheni hiyo ili kasoro zilizojitokeza katika awamu ya kwanza zisirudiwe,   pia kwa kuonyesha bayana kuelewa ukubwa wa tatizo na changamoto itakazopambana nazo wakati wa utekelezaji. Hii ni pamoja na kubuni mbinu na mikakati mipya ya utekelezaji na kuhakikisha zoezi zima linaendeshwa kwa kuzingatia haki za binadamu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema juzi wakati akitangaza kuanza kwa operesheni hiyo kuwa, Serikali inatambua kwamba inapambana na watu wenye nguvu kubwa, ikiwa ni pamoja na majangili na wafadhili wa mtandao wa biashara ya pembe za ndovu. Alisema watawakamata kuanzia maporini, ofisini na hata majumbani. Hiyo ni kauli nzito inayoashiria kwamba Serikali mara hii pengine inayo dhamira ya kweli ya kutokomeza vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa, kwani operesheni iliyopita ilihujumiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali, ambao wao binafsi ama ndugu zao walikuwa wakihusishwa na ujangili.
Miezi mitatu sasa baada ya kusitisha operesheni ya awali, tuhuma bado zimepamba moto kwamba mikakati ya kuwang’oa mawaziri ambao wizara zao zilihusika katika utekelezaji wa operesheni hiyo zilisukwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wakihusishwa na ujangili, huku wengine kadhaa wakidaiwa kufanya hivyo kwa masilahi binafsi ya kisiasa.
Kutokana na Kamati ya Kudumu ya Bunge kuliambia Bunge kwamba inayo majina ya wabunge na wanasiasa wanaotuhumiwa kujihusisha na ujangili, wananchi wengi sasa wanataka operesheni hiyo mpya isianze kabla majina ya watu hao hayajawekwa wazi, vinginevyo operesheni hiyo itaonekana kama kiini macho.
Ni kwa sababu hiyo tunaitaka Serikali mara hii isiwe na mzaha katika kuendesha operesheni ijayo. Kwa upande mmoja iwaondoe wakulima na wafugaji ndani ya hifadhi, kwani nchi yetu inayo ardhi ya kutosha nje ya hifadhi hizo kwa shughuli za kilimo na ufugaji. Ukweli ni kwamba wananchi hao ndiyo mawakala wa majangili wakubwa wanaomaliza tembo na maliasili nyingine. Pili ihakikishe  makazi ya watu yako mbali na hifadhi, kwani imegundulika wengi wa wafanyabiashara na wanasiasa wanaoishi karibu na hifadhi hizo nchi nzima wanajihusisha na ujangili na kwa kiasi kikubwa ndiyo waliofadhili njama za kuihujumu operesheni iliyopita.
Wakati tukisubiri uundwaji wa Tume ya Kimahakama kushughulikia ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa  operesheni ya awali, tunawataka wanasiasa, wakiwamo wabunge waiache Serikali itekeleze wajibu wake katika operesheni itakayoanza hivi punde. Baadhi ya wabunge waliopinga operesheni hiyo wanahusika na ujangili. Pengine ndiyo maana wananchi hawana tena shauku ya kuona Tume  ya Kimahakama ikiundwa.

UMAKINI WAHITAJIKA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI AWAMU YA PILI

Tokomeza ujangili awamu ya pili ifanyike kwa umakini zaidi

5th February 2014

Katuni
Juzi, serikali ilitangaza nia yake ya kuanza upya kwa `Operesheni Tokomeza Majangili' wakati wowote.

Tangazo hilo lilitolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kwenye mkutano ulioikutanisha serikali, mabalozi wa nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa.
Hata hivyo, Waziri Nyalandu hakutaja siku maalum ya kuanza kwa operesheni hiyo ya awamu ya pili.

Kwa mujibu wa Waziri Nyalandu, operesheni ya awamu hii itawakumba watu wote wanaojihusisha na  ujangili pamoja mitandao ya biashara za pembe za tembo na faru na kwamba itafanyika kwa nguvu kuanzia porini, ofisini hadi majumbani.

Aidha, alisema serikali imefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa opereshehi hiyo baada ya kusitishwa Oktoba 31, mwaka jana.

Operesheni ya mwaka jana ilisitishwa kutokana na malalamiko ya kuwapo kwa vitendo vya ukatili, mateso, mauaji ya wananchi wasio na hatia pamoja na upotevu wa mali zikiwamo fedha na mifugo.

Hali hiyo ilisababisha aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, kujiuzulu kutokana na shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge na wenzake watatu kutenguliwa uteuzi wao.

Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Jakaya Kikwete ni pamoja na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Dk. David Mathayo David (Mifugo na Uvuvi).

Sisi tunaunga mkono operesheni tokomeza majangili iendelee kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa hili kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Hali kadhalika, tunakubaliana na Waziri Nyalandu kuwa katika operesheni ya safari hii, serikali itapambana kikamilifu na maadui wakubwa ambao ni watu wanaotumiwa kuua wanyamapori na wafadhili wa mitandao.

Aidha, tunaamini kwamba ahadi ya Waziri Nyalandu kwamba katika zoezi hilo, dosari zilizotokea awali zitaepukwa na kuhakikisha kuwa operesheni hiyo ya awamu ya pili inafanyika kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Tunakubaliana na Waziri Nyalandu kuwa ni muhimu zoezi hilo likafanyika kwa weledi na ufanisi mkubwa ili kuepuka dosari zote zilizojitokeza katika operesheni ya kwanza ambayo kwa hakika iliitia doa serikali.

Tunafamu pia wazi kwamba hata operesheni ya kwanza, lengo lake lilikuwa ni jema lakini ilitiwa dosari na baadhi ya watendaji ama kwa makusudi, uzembe  au kwa kutojua athari ya walichokuwa wakikifanya.

Mathalani, tumeambiwa na mmoja wa askari aliyeshiriki awamu ya kwanza ya operesheni hiyo kwamba licha ya kuwa na nia nzuri ya kutokomeza ujangili, lakini usimamizi haukuwa mzuri kutokana na mamlaka zote za utawala zilizohusika kukosa uratibu.

Tunaamini kwamba operesheni ya sasa serikali itakuwa imejipanga vilivyo ili kuhakikisha kwamba dosari kama hizo na nyinginezo, hazijitokezi tena.

Tunataka operesheni ya awamu hii, ifanye kazi kwa lengo lililokusudiwa na pasipo kumuonea ama kumwandama mtu yeyote asiyehusika.

Kama itafanyika kwa weledi kama alivyoahidi Waziri mwenye dhamana, Nyalandu, kwa hakika kila mwananchi ataifurahia na kila mtu atakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa watendaji watakaopewa jukumu hilo zito.

Na kwa msingi huo, tungependa zoezi hili liwe rafiki kwa wananchi badala ya kuwa adui.

Aidha, pamoja na hayo, vile vile tungeshauri askari wote watakaofanya kazi hiyo, walipwe posho zao stahiki na kwa wakati badala ya kubaki wakilalamika.

Askari wasipolipwa stahiki ya posho zao, ni rahisi kurubunika na wakajikuta wanajiingiza kufanya  vitendo kinyume na adidu zao za rejea ama kuwafisha mioyo ya kufanya kazi hiyo.

Hii inatokana na ukweli kwamba askari walioshiriki operesheni ya awali, bado wanaidai serikali kiasi cha Sh. bilioni 1.5.
CHANZO: NIPASHE

Saturday, February 1, 2014

Wakamatwa na meno ya tembo


Jumamosi, Februari 01, 2014 09:20 Na Walter Mguluchuma, Katavi
WATU wawili  wakazi  wa  Mtaa wa Kawajense, Wilaya  ya  Mpanda, Mkoa  wa Katavi, wamekamatwa  kwa  tuhuma  za  kukutwa na  vipande   vitatu  vya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 24. Kamanda  wa Polisi Mkoa  wa Katavi, Dhahiri  Kidavashari, aliwataja  watuhumiwa hao kuwa ni Mateso Kayanda (35) na Damiani Kayanda (28).

Kamanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa jioni ya Januari  29, mwaka huu, nyumbani kwa watuhumiwa hao.

Kidavashari  alieleza kuwa watuhumiwa walikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba watu hao wanajihusisha na biashara haramu na ndipo jeshi likaweka mtego kuwanasa.

Alieleza siku ya tukio watuhumiwa walikamatwa wakiwa na vipande vitatu vya meno ya tembo vya thamani iliyotajwa.

Alisema watuhumiwa hao pia walikutwa na mbao 53 aina ya kipilipili za thamani  ya Sh. 250.000, ambazo walikuwa wakizimiliki  isivyo halali.

Kamanda Kidavashari alieleza watumiwa wanatarajiwa kufikishwa  mahakamani  mara baada ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika.

Bottom of Form