Sunday, August 26, 2012
Friday, August 24, 2012
Kagasheki aongeza uwazi Malisili
Kagasheki aongeza uwazi Malisili
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa bodi mbalimbali zilozopo chini ya Wizara hiyo.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Wizara hiyo, Bw. George Matiko, ilisema kuanzia sasa wajumbe wa bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.
Alisema hivi sasa kuna bodi nane zilizopo chini ya Wizara hiyo ambazo zimemaliza muda wake au kukaribia kuisha.
Aliongeza kuwa, bodi hizo ni za Taasii za Mashirika ambazo ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Taasisi ya Utafiti wa Misitu nchini (TAFORI), Makumbusho ya Taifa, Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA).
Bodi nyingine ni Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi, Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA) na Leseni za Utalii (TTLB).
Bw. Matiko aliwataka Watanzania wenye sifa za kuwa wajumbe wa bodi hizo, kupeleka maombi yao kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii. Baadhi ya watu ambao wamezungumzia hatua hiyo, walisema ni nzuri na imezingatia uwazi kupata wajumbe hao.
Source: Majira
Thursday, August 23, 2012
Waziri Kagasheki
Waziri Kagasheki amng'oa mkurugenzi wanyamapori
MKURUGENZI wa Wanyamapori katika Wizara ya Maliasiali na Utalii,
Obeid Mbangwa na wenzake wawili, wamefukuzwa kazi kwa kashfa ya kutorosha
wanyama hai 136 wa aina 14 tofauti kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) usiku wa Novemba 26, 2010.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya tume mbili zilizoundwa kuchunguza
suala hilo bila kuhusisha wizara yenyewe, kumaliza kazi yake na kukabidhi
ripoti kwa Waziri.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema
jana mjini Dodoma kuwa mbali na watuhumiwa hao, mtumishi mwingine wa wizara
hiyo amevuliwa madaraka, wawili wamepewa onyo kali la maandishi na wawili
uchunguzi dhidi yao unaendelea.
Mbangwa wakati wa kashfa hiyo ya kusafirisha wanyama hai
wanaokadiriwa kuwa na thamani ya Sh170 milioni kwa ndege ya kijeshi ya Qatar, alikuwa Mkurugenzia Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori.
Wengine waliotumuliwa kazi ni Simon Gwera na Frank Mremi waliokuwa
maofisa Uwindaji wa Kitalii, Cites na Utalii wa Picha mkoani Arusha.
Mkurugenzi Msaidizi, Uendelezaji Wanyamapori, Boneventura Midala
amevuliwa madaraka kutokana na kutochukua hatua kikamilifu za ulinzi ambazo
zingeweza kuzia kutokea kwa utoshaji wa wanyama.
Wakati tukio hilo alikuwa kurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Kuzuia
Ujangili.
Katika hatua hizo, maofisa wanyamapori Daraja la pili wawili
waliotekeleza maelekezo ya wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha sheria wamepewa
onyo kali la maandishi.
Kagasheki aliwataja kuwa ni Martha Msemo, Ofisa Leseni ya Uwindaji
wa Kitalii, Cites na Utalii wa Picha Arusha na Anthonia Anthony ambaye ni Ofisa Leseni Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, Cites na Utalii
wa Picha Dar es Salaam.
Rungu la wizara hiyo pia limemwangukia Mkuu wa Kituo cha uwindaji
wa kitalii, Cites na utalii wa Picha Arusha, Silvanus Ukudo aliyepewa onyo kali
la maandishi kwa kushindwa kufuatilia kupata maelekezo ya mkurugenzi wa
wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka sheria katika utoaji wa vibali.
Ukudo pia ameonywa kwa kushindwa kupeleka kwa katibu mkuu taarifa
kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za kinidhamu.
Kagasheki alisema uchunguzi unaendelea dhidi ya watumishi wengine
wawili, Mohamed madehele, Ofisa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na Mariam Nyallu, Ofisa wa kituo cha Uwindaji wa Kitalii, Cites na
Utalii wa Picha Arusha.
Alisema kwa upande wa wafanyabiashara waliohusika katika kashfa
hiyo, kesi inaendelea mahakamani, na kwa upande wa Qatar, Serikali inaendelea
kusubiri majibu, japo ni kwa muda mrefu, kwa kuwa Serikali ya nchi hiyo imendelea kukaa kimya.
“Tumefanya kila jitihada, tumewasiliana kupitia Makao Makuu ya
Cites, Geneva, Uswis, lakini Qatar pamoja na kukubali kupokea maombi yetu kutoka Cites, imekaa kimya,” alisema Kagasheki.
Kuhusu hatua zaidi dhidi ya watuhumiwa hao, Waziri Kagasheki
alisema, “kwa kuwa imebainika walihusika na vibali vilisababisha hao
wafanyabiashara wakamatwe walivitoa wao, suala hilo halijaishia hapo.”
Waziri huyo alisema atajitahidi kadiri ya uwezo wake kusimamia
wizara hiyo ili kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa.
“Sheria zipo nzuri, udhaifu mkubwa ni kwa watendaji wetu,”
alisema.
Kauli ya Mbangwa
Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo Mbangwa
alisema hajui chochote.
Alisema hadi jana alikuwa hana taarifa za
kufukuzwa kwazi hivyo hawezi kusema chochote hasa bila ushahidi.
“Unasema wamenifukuza kazi, ndo wametangaza
hivyo? Mimi sina taarifa hizo na hivyo
siwezi kuelezea chochote”alisema Mbangwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)